Na.Hillary Shoo.
Arusha.
WAKATI Timu ya soka ya Mkoa wa Singida ,Kindai Shooting Stars inatarajiwa kushuka dimbani leo kuumana na timu ya Mkoa wa Kisoka wa Ilala katika robo fainali ya Killi Taifa Cup, Mkoa huo umeendelea kuandamwa na msiba wa wachezaji baada ya mchezaji wa timu ya soka ya Mughanga Fc kufariki dunia ghafla.
Mchezaji huyo ambaye alikuwa akicheza nafasi ya beki wa kati ni Mussa Haruna (17) ambaye alifariki akiwa nyumbani kwao eneo la Mitunduruni Manispaa ya Singida.
Akizungumza mjini Arusha jana Katibu Mkuu wa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Singida (SIREFA ) Hussein Mwamba alisema kuwa mchezaji huyo amefariki dunia akiwa usingizini.
Mwamba alisema alipata taarifa jana asubuhi kutoka kwa baba yake mzazi ambaye pia ni mwamuzi daraja wa kwanza Mkoa wa singida,Haruna Kabombwe juu ya kifo cha mwanae huyo.
Alisema marehemu musa alikuwa alicheza ligi ya Taifa ngazi ya mkoa wa singida iliyomalizika mapema mwezi Machi mwaka huu na timu yake ya Mughanga ilishika nafasi ya tatu baada ya kufungwa katika nusu fainali na Aston Villa 2-0.
Aidha Mwamba alisema Mchezaji huyo Chipukizi mara baada ya kumalizika kwa ligi hiyo ya Taifa ngazi ya mkoa jopo la wataalamu wa soka mkoa walimchagua katika timu ya mkoa wa singida Kindasi Shooting Stars katika orodha ya wachezaji 30.
Hata hivyo alisema mchezaji huyo alichujwa kati ya wachezaji 10 kutokana na kuwa majeruhi ya goti ambapo kocha wa kindai Shooting Stars Abdala Msamba alimtoa katika orodhja way wachezaji hao na kubaki na kikosi cha cha wachezaji 20 kuunda Kindai Shooting Stars.
Marehemu alianza kiucheza soka akiwa katika shule za msingi umitashumta na baadae alichaguliwa kuunda timu ya copacoca cola kabla ya kujiunga na mughanga mwaka jana na kucheza ligi Taifa ngazi ya mkoa akiwa na timu yake hiyo.
Huyu ni mchezaji wa pili kufariki ghafla katika kipindi kisichozidi wiki tatu ambapo Mei 02 mwaka huu iliondikewa na mchezaji wake mahiri wa timu ya mkoa Kindai Shooting Stars Nassoro Issa (19) wakati akiwa kwenye mazoezi uwanja wa mwenge sekondari akiandaa na mashindano hayo ambapo Kindai ilikuwa kituo cha Tabora na kuibuka washindi wa kwanza kituo hicho.
Meneja wa timu ya mkoa wa singida, Muna Dawood kwa niaba ya wachezaji wa timu ya mkoa ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mcherzaji huyo na kusema kuwa wamesikitishwa na Msiba huo kipindi hiki kigumu ambacho timu iko mashindanoni Mkoani Arusha.
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya mchezaji Mussa Haruna.
Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe, AMEN.







