UKAME NCHINI SOMALIA WAENDELEA KUUA MAELFU YA WATU.

Mamia ya wakazi wa Somalia walioathirika na janga la ukame wakiwa wamekusanywa katika eneo la kupewa misaada.

Na.MO BLOG TEAM

Ukame nchini Somalia umeendelea kusambaa katika maeneo  ambayo hata awali hayakuwa  maeneo hatari  kwa ukame, na kuacha maelefu ya familia wakihangaika na kutojua la kufanya.

Julai  kumi na Moja –makundi ya kijamii yalifanya matembezi ya pamoja kwaajili ya kusaidia watu walioathirika zaidi na walio katika hatari ya vifo vilivyokuwa tishio vinavyotokana na hatari ya kusamba kwa ukame nchini Somalia. Na kuhusisha na kuongezeka kwa idadi ya vifo vinavyotokana na njaa.

“Tumekuwa tukibisha hodo kila mlango kwa lengo la kukusanya chochote kitachopatikana kwani kwentu hakuna kidogo kwaajili ya kusaidia, alisema haya mjimbe wa kamati ya kundi la kijamii ya kusaidia tatizo la Ukame , Asha Sha’ur Ugas.

Mjumbe huyo aliongeza kuwa “watu wengi tayari wameshafariki dunia na wengine zaidi wanaweza kufa kama msaada hautawasili kwa haraka na kwa maana ya haraka ni sasa.”

Amesema,” wameshapokea ripoti tayari  ya watu waliopoteza maisha wakiwa njiani na wengine waliofariki  baada ya kuwasili kwenye mji mkuu wa MOGADISHU”, NA KUONGEZA , “wengi wa waliopoteza masiha ni watoto na watu wazima waliokuwa dhaifu sana sambamba na wazee na wajawazito na wakina mama wanaonyonyesha”.

Mjumbe huyo amesema, Makundi hayo ya kijamii yamepeleka ombi rasmi kwa wasomali waliopo nchini na watu wa nje ya nchi hiyo kusaidia, na kwamba ndani ya  Mogadishu,watoto wa  shule,wanwake wafanyabishara  sokoni ,sambamba na wafanyabiashara wamekuwa wakichangia chochote wanachoweza.

Amesema Makundi hayo ya kijamii yanajiandaa kupeleka misaada ya kijamii katika eneo lolote au ukanda wowote ulioathirika ,bila kujali nani anadhibiti eneo hilo.Ameongeza “ Tunajiandaa kwenda popote katika nchi hii kama itaweza kuwa msaada ambao unatakiwa.”

 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional