Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salimu akizindua maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho jijini dar es salaam. Chuo hicho kianzishwa tarehe 29 Julai mwaka 1961.Wageni wengine ni pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba .
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni Dkt. John Magotti akitoa hotuba ya ukaribisho jana jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uanzishwaji wa Chuo hicho.
Mawaziri Wakuu Wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba (kushoto) na Dkt Salim Ahmed Salimu(kulia) wakibadilishana mawazo jijini Dar e salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uanzishwaji wa Chuocha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kivukoni.
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa mada juu ya mchango wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika maendeleo ya ya Taifa jijini Dar es salaam wakati wa uzindua maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho . Chuo hicho kianzishwa tarehe 29 Julai mwaka 1961.
Wanajumuiya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni wakimsikiliza kwa makini hotuba ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho iliyotolewa jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim (hayupo pichani).
Wanajumuiya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere , Kivukoni wakicheza muziki jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho .(Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es salaam)














at 3:14 pm
nafkir mngetupatia na hotuba yake ingekuwa vizuri zaidi.