SALHA ISRAEL ATWAA TAJI LA VODACOM MISS ILALA 2011.

Mmoja wa washiriki wa Miss Ilala akionyesha kipaji chake cha kuchezea nyoka katika shindano la kumtafuta Miss Ilala ambapo Salha Israel ndiye alieibuka kidedea katika shindano hilo na kujipatia tiketi ya kushiriki shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011.

Warembo tano bora walioingia katika shindano la kumtafuta miss Ilala Julai 29, 2011, Mrembo Salha Israel ndiye alieibuka kidedea na kujipatia tiketi ya kushiriki shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011,Shindano hili lilifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.

Mrembo Alexia William akijibu swali na kuweza kujipatia ushindi wa namba mbili na kuweza kujikatia tiketi ya kushiriki shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011.

Ofisa udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude akimpongeza Miss Ilala Salha Israel mara baada ya kutangazwa mshindi na kujikatia tiketi ya kushiriki katika shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania pamoja na wenzake mshindi wa pili na watatu.Shindano hili lilifanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Miss Ilala 2011 Salha Israel (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na warembo wenzake msindi wa pili Alexia William kusho na mshindi watatu Jenifer Kakolaki kulia waliojipatia tiketi ya kushiriki shindano la kitaifa la Vodacom Miss Tanzania 2011.

 


 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional