Mbunifu wa Mavazi Mustafa Hassanali kutokaTanzania, akiongozana na mmoja wa wanamitindo kuonyesha vazi la ubunifu katika hafla ya Fashion Week nchini Gaborone,Botswana 13 August 2011.
Pichani Juu na Chini ni wanamitindo wakionyesha vazi la ubunifu la Mustafa Hassanali kutoka Tanzania tarehe 13 august-2011 wakati alipofanya onyesho nchini Gaborena Botswana.
Na.MO BLOG TEAM
Mbunifu Mtanzania Mustafa Hassanali, ameiwakilisha Tanzania katika Maonyesho ya wiki ya kwanza ya Fashion Botswana, yaliyofahamika kama Color in the desert fashion week.
Katika Maonyesho hayo wabunifu mbalimbali wa kimataifa na wenyeji walihudhuria.
Baadhi ya wabunifu wa kiafrika waliohudhulia ni pamoja na Taibo Bacar (Mozambique), David Tlale,na Thula Sindi kutoka Afrika kusini, Moo Cow (Kenya), na Joyse Nyasha Chimanye wa nchini Zimbabwe.
Kauli mbiu ya Fashion week mwaka huu,ilikua “Kuongeza tija na maendeleo ya fani ya ubunifu wa mavazi na viwanda vya nguo Botswana”
Akizungumzia Maonyesho hayo Mustafa Hassanali alisema “Kutokana na uzoefu wangu,Botswana ni nchi yangu ya kumi na moja kiafrika na ya kumi na tatu kidunia kufanya maonyesho ya ubunifu,Na ninajisikia faraja na kujivunia kuwa mmoja wa waliohudhuria week ya kwanza ya fashion Botswana,na pia kuwa mmoja wa kuendeleza uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Botswana kupitia Fashion. “











