MTOTO SESILIA EDWARD – KUSAFIRI JUMATANO NCHINI INDIA TAYARI KWA UPASUAJI WA MOYO.

Pichani ni Mwendesha kipindi Nani ni Nani kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Channel Ten Hoyce Temu(kulia) akimfariji mtoto Sesilia Edward ( wa pili kulia) Mwenye matatizo ya Moyo anayehitajikwa kufanyiwa upasuaji wa Haraka nchini India.

Ndugu Watanzania,

Shukrani za pekee ziwaendee wale wote waliojitolea kwa hali na mali kumchangia mtoto Sesilia Edward ambaye anahitaji msaada wa haraka wa operesheni ya moyo.

Tunapenda kuwataarifu kuwa fedha za operesheni zimekwishapatikana, na tayari tiketi mbili (ya kwake na mlezi wake Peter Nyambaliko) zimekwisha patikana.

Kwa sasa, mtoto Sesilia amelazwa katika hopsitali ya Regency chini ya uangalizi mkubwa wa Daktari Bingwa Dr. Kanabar na timu yake tayari kupunguza maji yalioyojaa tumboni kabla ya yeye kusafiri siku ya Jumatano.

Dola 6,100 tayari zimekwishalipwa kwa ajili ya matibabu India, na tiketi mbili zimekwishalipiwa. Tayari tumelipa shilingi 200,000 kama admission fee katika hospitali ya Regency ambapo tunatemegemea mtoto Sesilia atalazwa hadi Jumanne tarehe 20, kabla ya kusafiri Jumatano. Gharama zilizobaki za Regency zitagaramiwa na hospitali ya Regency. Yote hii ni katika kuiweka hali yake sawia kabla ya safari ndefu kuelekea India.

Bado tunahitaji msaada wa fedha za kununua madawa ambapo kwa wiki mtoto Sesilia hutumia madawa zaidi ya shilingi 50,000. Tunahitaji nguo kubwa kubwa za kuvaa kwani tumbo linaongezeka sentimeta moja kila baada ya masaa 72.

Unaweza kumtemebelea mtoto Sesilia katika hospitali ya Regency kwa  leo jumatatu na kesho jumanne

Kama una msaada wa haraka kama nguo, chakula peleka katika kituo cha Chanel Ten – Dar es Salaam.

Na weka pesa katika account zuatazo:

Tigo Pesa:-  0715 095797

MPESA:  –  0762 962467

NMB Account: 2072517079

Kwa maelezo zaidi, piga simu 0767-262625

Watanzania tumeweza, tunamuombea mtoto Sesilia aende salama na arudi salama.

Shukrani za dhati kwenu wote kwa niaba ya Africa Media Group Limited

Hoyce Temu

Mtangazaji  – Mimi na Tanzania.

 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

1 Comment

  • Jaliath

    nimefatili matataizo na matibabu ya mtoto Cecilia. nimeona amerudi na hakuna mafanikio kama tulivyo taraji.

    natoa ushauri kwa Hoyce Temu, kwa Mungu hakuna kinachoshindikana. mimi natazama sana Emmanuel TV kupitia dish la media com, au mfatilie kama humfahamu, tafadhali itafutwe pesa ili aende Nigeria, i am sure 100% atarudi amepona kabisa. yani please usipuuze hilo.

    Mungu anatenda!

    Jaliath

     
 

 

Add a comment

required

required

optional