KATIKA baadhi ya vyombo vya habari jana na leo, kumeripotiwa taarifa za kuwapo kwa ugomvi baina ya wachezaji wawili wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi na Haruna Moshi Shaaban (Boban).
Ugomvi huo umeripotiwa kutokea mara baada ya pambano la watani wa jadi lililofanyika jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Vyombo hivyo viliripoti kuwa chanzo cha ugomvi huo ni madai ya hujuma na kutoaminiana ndani ya timu.
Kwa masikitiko makubwa, Simba Sports Club (SSC) inapenda kukanusha kwa nguvu zote kuwapo kwa ugomvi wa aina yoyote baina ya wachezaji au viongozi wa klabu mara baada ya pambano la jana.
Mara baada ya mechi, hali iliyotamalaki ilikuwa ni ya fadhaa na huzuni kwa wote wanaohusika na Simba, wakiwamo wachezaji na washabiki.
Habari hizo za ugomvi wa wachezaji ni uzushi unaoenezwa na watu wasioitakia mema SSC.
Kuna mambo mawili yanayoweza kubainisha kuwa habari hizo hazikuwa za ukweli. Kwanza, kwamba vipo vyombo vilivyodai kuwa Okwi alipigwa hadi kuvimba uso. Ukweli ni kuwa Okwi yuko salama, buheri wa afya na hajavimba popote mwilini mwake, achilia mbali usoni.
Pili, kuna magazeti yaliyoandika kuwa Okwi alipigwa vichwa vinne Boban kabla hawajaamuliwa. Mengine yakaripoti kichwa kimoja. Kuna redio imeripoti kuwa vilikuwa vichwa vitatu. Tukio moja, taarifa tofauti lukuki.
Kikubwa ni kuwa, hakuna mwandishi wa habari hata mmoja aliyeshuhudia tukio hilo na kulithibitisha pasi na shaka zaidi ya kusimuliwa na wale waeneza uongo.
SSC inashukuru kwa ushirikiano mzuri inaopata kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje.
Tunawaomba wana Simba wawe watulivu katika kipindi hiki na tujipange kwa ajili ya mechi yetu ijayo ya VPL dhidi ya Moro United. Kama tutashinda, tutaongoza ligi hadi mwakani.
Timu inarejea kambini leo tayari kujiandaa na pambano hilo la mwisho la raundi ya kwanza ya VPL.
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
SSC.











at 3:14 pm
simba itaendelea mbele kwa vyovyote watakavyosema huo ndio msimamo “uzushu hauwezi kuwafanya wanafamilia kutengana kwa vyovyote vile”
at 12:14 pm
simba mbeleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee daima
at 12:16 pm
simba mbeleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee daima
at 12:41 pm
Tunapenda tupate habari za club yetu ambazo ni latest pia tuboreshe WEB SITE yetu iendane na wakati kila mwana simba apate habari za club kwa wakati
at 12:43 pm
wimbo wetu wa eeeee kidedea ndo wimbo wa taifa la msimbazi hakuna haja ya kuhangaika kupata wimbo mpya
at 10:50 am
Simba kama man u yan mixer tv simba 4rever
at 1:58 pm
Tunamuombaa mungu we2 hi ndo nymbo nzur kwa wana msimbaz coz 2namuomba mwenyz mungu so hatutak kuchange nymbo,simba mbeleeeee.
at 6:09 pm
hey i would like to join simba sc soon after finishing form four this year so i was requesting for this chance because i hope that i will be helpful in our team i need a chance people.
at 8:10 pm
Kiukweli kwa sasa tuna timu nzuri saana! Mungu atuepushe na roho ya majungu na ubinafsi hili tutwae hili kombe la shirikisho afrika na ligi kuu bara.
at 11:24 am
Kweli simba ni miamba ya Afrika mashariki na kati.Viongozi,mashabiki,pamoja na wachezaji tuwe kitu kimaja kuiendeleza club yetu.simba juuuuuuuuu!
at 11:26 am
simba juuuuuuuuuuuu
at 8:11 am
Mimi ni mwanachama card no02002 Napongeza wachezaji wote pamoja viongozi kwa ushindi mnono w-WITO tUSHIKAMANE
at 8:13 am
Mimi ni mwanachama card no02002 Napongeza wachezaji wote pamoja viongozi kwa ushindi mnono WITO tUSHIKAMANE
at 10:15 am
poleni sana kwa msiba
at 3:35 pm
WANA SIMBA TUMUOMBEE PATRICK MAFISANGO APUMZIKE KWA AMANI. TUJIPANGE KWA MSIMU UJAO. VIONGOZI WAAANDAE TIMU YETU MAPEMA
at 7:26 pm
plen sana wanasimba wenzangu kwa kuondokewa mchezaji wetu mahili Patrick Mafisango na Mungu aiweke roho ya marehem mahali pema peponi Amina.
at 6:12 am
POLENI WANA SIMBA KWA MSIBA WA MAFISANGO KWELI LIMEKUWA NI PIGO KUBWA SANA TUJIPE MOYO KATIKA KIPINDI HIKI KIGUM,BWANA AMETOA BWANA AMETWA JINA LAKE LIHIMIDIWE DAIMA.