-AZUNGUMZA NA MO BLOG NA KUWEKA WAZI MIKAKATI YAKE IJAYO.
-ASHAURI ABIRIA KUFAHAMISHWA MBINU ZA KUJIOKOA.
MO BLOG : Wewe ni mtangazaji wa vipindi vya televisheni na mara ya mwisho umeonekana katika kipindi cha ‘Uwazi’ kilichokupatia umaarufu mkubwa sana. Kwa sasa uko wapi na unafanya nini?
MUSSA HUSSEIN: Kubwa zaidi ilikuwa ni maandalizi tu, kutoka kwenye ‘Uswazi na kuingia hatua nyingine. Uswazi ilikuwa ni mwanzo tu lakini sasa hivi tunaingia kwenye hatua nyingine ya kuwathibitishia wananchi kuwa inawezekana tuwaonyese maisha ya watu ambao unawaona wapo, lakini katika maisha yao hujui wanaishi vipi wala wanamtazamo gani. Nilipokuwa nikizungumzia maisha ya ‘Uswazi’ kila kilichokuwa kikizungumzwa ni kuhusu mambo mabaya mabaya tu, lakini kweli hakuna mazuri..? jibu ni kuwa yapo..!!
MO BLOG : Kwa maelezo hayo unataka kutuambia nini.?
MUSSA HUSSEIN: Maana yangu ni kwamba sasa tunataka kuwaonyesha wananchi kuwa katika maisha, mema pia yapo na sio mabaya peke yake. Na pia tunataka kuwafunulia watazamaji ukweli zaidi maana stori za kwenye ‘Uswazi’ zilikuwa za kusimuliwa zaidi. Yaani maana yake ni kwamba unaona kwa undani tukio lenyewe lilivyotokea na tutakuwepo eneo lenyewe na sio kusimulia.
Mara ya kwanza nilikuwa sikuonyeshi mwisho wake ni nini lakini this time sikuachi njiani wala sikuachi na shaka nakuonyesha mpaka mwisho wa tukio ulivyokuwa.
MO BLOG: Sasa maana hiyo tumeelewa kuwa unaandaa kipindi kipya kitaitwaje? Na kitazungumzia tukio gani..?
MUSSA HUSSEIN: Kipindi nitakacho anza nacho kitaitwa ”Safari Ya Nungwi” na kitazungumzi hali halisi ya matukio yaliyojiri wakati ilipotokea ajali ya kuzama kwa meli kule Nungwi Zanzibar.
MO BLOG: Nini kitakuwa tofauti na vipindi vingine vya TV ambavyo umewahi kufanya.?
MUSSA HUSSEIN: Kitu ambacho kitakuwa tofauti na show nyingine ambazo mimi nimewahi kufanya ni kwamba hapa nitakupa stori za ajali za kuzama kwa meli sio ya Nungwi pekee bali hata zilizopita nikikuonyesha matukio yenyewe yalivyokuwa tofauti na unaposoma kwenye gazeti au kusikia redioni. Kwa mfano katika taarifa ya habari utaonyeshwa kwa sekunde 30 tu mchezo umekwisha.
Hivyo huwezi kugundua haya matukio ni makubwa au ni madogo kiasi gani.
MO BLOG: Nini kimekufanya ufikie maamuzi ya kufanya kipindi cha namna hii kinachoonyesha matukio halisi au huridhishwi na jinsi taarifa za majanga zinavyotolewa?
MUSSA HUSSEIN: Kwanza watanzania hatuna utamaduni wa kusoma, ila ninachoshukuru Mungu kwa sasa hivi kuna ongezeko kubwa la watanzania wanaotazama TV au mitandao hii mingine iliyopo, kwa kutokea hapo nikaona kwa sababu kila siku tunatoa lawama kwa serikali wakati mwingine tunalaumiana wenyewe kwa wenyewe ipo haja ya kupeana elimu wenyewe kuhusiana na majanga yanayotokea kila mara ikiwemo kwenye maji, barabarani au popote pale.
Kwa sababu kila siku anayeandika anasema Ajali za Barabarani zitatumaliza, Ajali za angani zitatumaliza, Ajali za majini zitatumaliza kila siku ni hivyo hivyo. Na ukiangalia hizi ajali za sijui meli, treni, mabasi zinaua mamia ya watu.
MO BLOG: Mussa Mo BLOG inakupa ukumbi endelea kufunguka kama unavyotaka.!
MUSSA HUSSEIN: Lakini tukiangalia, je hakuna njia zozote tunazoweza kuzitumia kudhibiti hizi ajali? Kwa hiyo mimi hali hiyo ikaniuma nikaamua kufanya research kutaka kujua ajali inapotokea kwani inatokeaje?
Kwa mfano wakati inatokea ajali ya kuzama kwa MV Bukoba, Mimi niko nyumbani nasikia kwenye radio kuhusu ajali hiyo, natizama kwenye TV lakini sipati kuona kiundani kuwa tukio hilo je ni kubwa au ni dogo kiasi gani? Nini kimesababisha izame? Stori zinaishia kwenye magazeti na maneno ya mdomo.
Ndio suala la Nungwi nikaona kwamba tayari imetokea hivyo na mimi nilikuwepo eneo la tukio basi ngoja nifanyie kazi tukio hilo wananchi wapate kufahamu nini hasa kimetokea.
Sasa hii stori ya Nungwi tumetengeneza episode nne(4) kwa hiyo katika kipindi cha mwezi mzima tutakuwa tukisafiri kwenda Nungwi. Nitakuonyesha jinsi meli ilivyotoka Dar es Salaam mpaka ilipofika Unguja stori zipo na ilipotoka Unguja mpaka ikaenda kuzama Nungwi.
MO BLOG: Mussa baada ya kufanya research na kutengeneza Safari ya Nungwi umejifunza nini?
MUSSA HUSSEIN: Ndio kama vile nilivyosema mwanzo, mimi mgeni kwenye boti sijui dirisha la kutokea liko wapi wala mlango wa dharura uko wapi wala vifaa vya kujiokolea vinakaa wapi. Sasa meli hii ilipokuwa ikizama taa zilizima ghafla hakuna mtu aliyekuwa akiona kulia wala kushoto wala kujua ‘life jackets’ ziko wapi ..!!
“Ni sawasawa nikuingize ndani ya nyumba yangu kisha nizime taa halafu nikwambie kanichukulie kisu jikoni.”- utakuwa mtihani.
Kwa hiyo kuna vitu tumevigundua kuwa kwanini majanga yanapotokea yanakuwa makubwa zaidi kwetu. Ni kwamba hata zile mbinu za kujiokoa hatuzijui kwa sababu hatujapewa zile basics kwamba if anything happens you can do ABCDEF…!! Kujisalimisha before mtu mwingine hajaja kukupatia msaada.
Hicho ndio kitu kilichosababisha kupoteza watu wengi sana katika ile ajali ya Nungwi.
MO BLOG: Nini kingine umegundua kuhusiana na ajali hii..?
MUSSA HUSSEIN: Jambo la pili ni udhibiti wenyewe. Watu wengi hapo tunaziacha mamlaka zinazohusika lakini mimi naona kinachotakiwa ni kubadilisha ‘attitude’ za watu. Udhibiti wa ukweli kabisa unaanzia kwako wewe mwenyewe kwanza, lakini kwenye safari ya Nungwi watu walikuwa wanategemea udhibiti wa serikali. Kiuhakika usalama unatakiwa kuuanza wewe. Ukiangalia katika ile ajali waliokufa wengi ni kina mama na watoto, lakini tujiulize kwanini kina mama na watoto..? na hili ndio jambo tunalolalamikia kila siku..tunagundua kuwa wangetoa wapi information za hatua za kuchukua kunapotokea ajali. Watoto ni kundi la watu ambao hawana hatia ambao walikwenda wengi sana katika ajali hiyo..lakini jiulize ni kwa sababu gani?..jibu ni kwa sababu hakuna sheria zinazowalinda watoto katika hivi vyombo.
Pia hakuna udhibiti wa mzazi kwa mtoto wake wala wa vyombo vyenyewe kwenda kwa mtoto.
Utaratibu uliopo kwenye ndege, mabasi na train unajulikana kuhusu watoto. Lakini utaratibu huu wa meli za kwenda Zanzibar ni kizungumkuti. Kwamba mimi nina watoto 9, mimi pekee ndio nitakayekata tiketi na watoto wote 9 watasafiri bure.
Kingine ni kwamba meli zinapopakia mizigo Zanzibar hakuna mizani inayoonyesha meli imepakia mizigo tani ngapi. Bali magari yanajaza mizigo yanapangwa tu ndani ya meli pale forodhani then wanaondoka.
Nnachojiuliza ni kuwa, sasa..! tunapima na nini mzigo kama huu?
Huko tunakokwenda sijui itakuaje? Maana kuna panton zinavusha watu kwenda na kurudi Kigamboni kila siku, hakuna tahadhari zinazochukuliwa, tunasubiri litokee la kutokea halafu tushushe bendera nusu mlingoti.
Kwa hiyo ndugu ya Lemmy na Zainul kubwa zaidi katika vipindi nitakavyokuwa nafanya nikianzia na Safari ya Nungwi ni kuonyesha ukubwa wa haya majanga yanayotokea….mimi nimemaliza.
MO BLOG: Unamalizia kwa kusemaje?
MUSSA HUSSEIN: Nasema hivi ili kujua nani wa kulaumiwa katika majanga kama haya ambayo yanajirudia kila baada ya muda kwanza jamii ianze kwa kutazama episode 4 za ‘Safari Ya Nungwi’ na kwa wale mabloggers wasisite kupia MO BLOG kila siku ili wahabarike na kuburudika na kisha kuelimika. Akshateni.
BUSARA ZA MO BLOG: inamtakia Mussa Hussein mafanikio katika lengo lake la kutaka kuielimisha jamii kuhusiana na masuala mbali mbali hasa kuionyesha uhalisia wa majanga ya ajali, nini kifanyike na sio kuanza kulaumianana na kumtafuta mchawi, kumbe mchawi ni wewe mwenyewe unayeona gari limejaa lakini unapanda halafu unasimama, hudai tiketi, wala kusajiliwa kwamba ulikuwemo ndani ya usafiri huo.















at 7:26 am
yaha nakukumbali kijana kwa kujituma kijana kwa kufuatilia maswala ya kijamiii hongera sana
at 9:42 am
Musa hajatuambia kipindi kitakuwa kikionekana TV gani???
at 12:45 pm
Shalom,pongezi kwa mussa,ukimya wake tunaamini unakuja na kishindo,ila anatakiwa kuchagua kituo chenye mvuto kwa vijana,hasiende vi-TV uchwara vinavyoishia kibaha hatakuwa hajawatendea haki watazamaji ambao walikuwa wakimpenda toka alipokuwa EATV,EATV inaonekana kenya,uganda na bongo nzima,sasa yeye ataonyeshea wapi (kituo) gani hicho kipindi chake?kama kupitia blog,kuna watazamaji wangapi wana uwezo wa kuangalia blog kila siku?kazi kwake….TAFAKARI NA CHUKUA HATUA……..Mdau…Pc makame-ITV.
at 3:46 pm
NAPENDA MAWAZO YAKO MAANA MIMI NIMPENZI WA VIPINDI ENZIHIZO UKO KWENYE KITUO FULANI,NATUMAINI MAWAZO YAKO NA LENGO LAKO LITAFANIKIWA NDUGU YANGU.
at 9:41 am
hongera sana Musa ila pia jaandae kukutana na upinzani wa kisiasa si unajua nchi yetu kila kitu sirikali.ila nakutakia mafanikio mema jitahidi urushe kupitia ITV or EATV zinaonekana mbali.good lucky.
at 5:52 pm
safi sana mussa kwa kazi yako nzuri. brother Dewij safi sana blog yako inatuelimisha sana
at 12:06 pm
all the mussa,mhhh n kweli jamii lazima ifahamu jinsi ya kujkomboa pindi ajali inapotokea