MATOKEO YA DARASA LA SABA 2011 YATANGAZWA.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo (kushoto) akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi uliofanyika nchini mwezi Septemba 2011 leo jijini Dar es Salaam. Katika matokeo hayo wanafunzi 567,567 kati ya 983,545 wamefaulu mtihani huo, wavulana wakiwa ni 62.49% na wasichana wakiwa 54.48% ufaulu ukiongezeka katika masomo ya kiingereza, Kiswahili, Maarifa ya Jamii, Sayansi na Hisabati huku wanafunzi 9736 wakiwa wamefutiwa matokeo yao mkoa wa Manyara ukiongoza.
(Picha na Aron Msigwa –MAELEZO).

(Na.Gradys Sigera & Magreth Kinabo – MAELEZO)

Jumla ya wanafunzi 567,567 wamefaulu mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011 na  watafanyiwa mtihani wa majaribio  kabla ya kuanza masomo yao rasmi katika shule walizochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Akitangaza matokeo hayo (leo), jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari,  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Philipo Mulugo (Mb.) amesema, utaratibu huo wa kufanyiwa majaribio utaanza mwakani  2012,  ambapo wanafunzi waliofaulu watafanyiwa majaribio ya kupima stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu.

Wakati huo huo, Baraza la Mtihani la Taifa limefuta matokeo yote ya watahiniwa 9,736 sawa na asilimia 1.0 waliobainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani huo.

“Mwanafunzi atakayebainika kuwa kajiunga na kidato cha kwanza bila kumudu stadi hizo, Mwalimu Mkuu wa shule alikotokea mwanafunzi huyo na Msimamizi wa Mtihani wakumaliza elimu ya msingi watachukuliwa hatua za kinidhamu,” amesema Waziri Mulugo.

Akizungumzia kuhusu kiwango cha ufaulu alisema kimeongezeka hadi kufikia  asilimia 58.28 ukilinganisha  na cha mwaka jana ambacho kilikuwa asimilia 53.52.

Aliongeza kuwa  kiwango cha ufaulu wa masomo ya Kiingereza, Sayansi na Hesabu  kimepanda . Somo la Kiingereza  kutoka  asilimia 36.47  mwaka jana hadi  asilimia 46.70 kwa mwaka huu , wakati somo la  Sayansi  ni asilimia  61.33 mwaka huu  toka  asilimia 56.05mwaka jana na Hesabu  asilimia 39.36 mwaka huu toka asilimia 24.70mwaka jana.

Jumla ya wanafunzi 983, 545 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwezi wa Septemba 2011 na kuonesha kuwa, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kutoka asilimia 53.52 mwaka jana hadi 58.28. Jumla ya wasichana waliofaulu ni 27,377 na wavulana ni 289,190.

Wakati huo huo,  Serikali imesema, kazi ya kuhakiki madai ya walimu imekamilika tangu Desemba 2, mwaka huu na kwamba madai hayo ni kiasi cha sh. bilioni 52.

Akijibu swali lililoulizwa na waandishi kuhusu madai ya walimu, Naibu Katibu Mkuu Bw. Selestine Gesimba amesema, kati ya fedha hizo, shilingi  bilioni 30 ni za mishahara na bilioni 22 ni za madai mengineyo.

Bw. Gesimba ameongeza kuwa, madai ya  malipo mengine yataanza kulipwa  mwezi huu (Desemba) na   madai ya malipo ya mishahara   yatalipwa  ifikapo Januari 2012.

Hata hivyo alisema tayari Hazina wameshalipa bilioni 28 za madai ya mishahara kuanzia Julai mwaka jana hadi Novemba mwaka huu.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

57 Comments

 • Mathias kasomeko

  Moderator habari haijakamilika. Yako wapi hayo matokeo, hayo yote uliyoyataja hapo juu ni mbwembewe tu? yametoka wapi? SAMora avenue, NECTA website? Haijabalance hii habari. Asante kwa Alert hata hivyo although umetuacha kwenye suspense..

   
 • Kiwango cha ufaulu cha darasa la saba kwa masomo ya hisabati sayansi na kingereza kimeongezeka sababu kuu ni kuwa mitihani ilikuwa ni kuchagua herufi sahihi.kuchagua herufi sahihi ni mchezo wa kubahatisha hivyo serikali itafute njia mbadala siyo kujidanganya hakuna kiwango chochote cha ufaulu kilicho ongezeka.

   
 • John phidel

  Hongereni walimu kwa kuwafundisha vijana kwa nguvu ndio sababu kiwango chakufaulu kimeogezeka kuliko mwaka 2010 .

   
 • Deograsias dismas.

  Dah!hivi walimu wa Grade A wataajiriwa lini?mbona wameachwa sana nyumbani bila ajira?
  Af matokeo kwa njia ya majina yanatakiwa yawekwe kwenye internet!sababu Hii ni dunia ya utandawazi bwana alaaaaaaa!!!!!

   
 • Matokeo ya darasa la saba vii 2011

   
 • Charlschillengas

  Dah! Matokeo ya mwaka huo,sio,mabaya sana wala amzuri sana..

   
 • akida

  inamaana kwamba hyao waliofaulu mtihani wa awali waaminiki ndo maana ya ya kufanya jaribio au kusema hamjiamini na kazi yenu??????????/

   
 • Hassan Ninga

  jamani wirara mtawapa presha waalimu wanajijua wamewachachulika wanafunzi wao ila mna lengo zuri wa kuwapata wasomi wenye sifa hongereni…………..

   
 • isaack

  mtihani wa hisabati darasa la saba ulikuwa kuchagua majibu sahihi hivyo haukuwa na ubora wowote. nashauri serikali isiweke majibu ya kuchagua mtihani wa hisabati na masomo mengine maswali ya kuchagua majibu yapunguzwe. halikadhalika serikali ilipe walimu nawataalamu wengine kama madaktari mishahara mizuri badala kuongezea wabunge posho. pia waziri wizara ya utumishi abadilishwe aliyeko sasa hafai angekuwa anapigiwa kura na watumishi yawezekana angekataliwa kwa asilimia mia. heri enzi za Mary Nagu

   
  • Selemani Mponda

   Kweli mambo yanabadilika cku hz enzi za Mwalimu watu tulikuwa tunasolve paper kwa swali,kazi,na jibu sasa hv watoto mnawapa kitonga cha kuchagua hapo ni wizi mtupu!

    
 • Hamna la maana ya kuweka matokeo mengine mfano form four or form six wakati ya darasa la saba hayawekwi kama vipi msiwe mnaweka kabisa ili tujue ya kuwa bado tupo kwenye early stone age.

   
 • kelvin mongomongo

  Tunaomba matokeo yawekwe kwenye intanert jamani bcuz huu ni wakati wa science and technology masuala ya mpaka kubandikwa yamepitwa na wakati,lakini ongeleni kwa kazi nzuri necta.kazi njema!

   
 • hongereni kwa kazi nzuri mliofanya walimu mungu awabariki ila majina ya waliofaulu yawekeni kwenye internet sio mpaka mbandike huu ni wakati wa science and technology so keep it up

   
 • JUMANNE

  mbona kumeandikwa maneno tu sisi tunataka tuyaone majina kwenye internet mbona tunaendeleza habari za zamani.

   
 • Matokeo ya darasa la saba kwa mwaka hu yana lidhisha sana baraza la mitihani liwe lina tunga mitihani ya muundo huohuo

   
 • kassim bwaki

  hayo ni mambo ya kizamani Mtihani mmoja kwa wanafunzi wote tanzania lakini mnashindwa kutuma matokeo katika intanet.

   
 • kennedy

  jamani mlisema miaka 50 ya uhuru mlithubutu mkaweza na sasa mnasonga its ok mmeweza kwa lipi sasa mbona hata kuweka matokeo kwenye net imewashinda????.then hao wanafunz mliowahukumu kwa kuwafutia matokeo yao kwa nini msingewapitisha wote then kabla hawajaanza form one wapewe mtihani wa mnchujo wote??? hamuoni kuwa mnawanyanyasa watoto kwa kipindi chote walipokuwa darasani kwa miaka saba mpaka hata 9 darasani.thats not fare….hata kama mnaboresha elimu.au kama walimu hamuwaamini kwanin msiunde chombo maalumu cha kusimamia mtihani tuuu???? then na kama lengo ni kuboresha elimu na kupata wasomi wazuri mbona bado mashule mengi hayana maabara na waalimu wa kutosha na wengine wanasomea chini ya miti wengine hawana madawati na vitabu??? au staili ya kuwafutia watoto matokeo na kuwaunmiza wazaz wao ndo njia ya kisasa ya kuboresha elimu ????

   
 • MARIAM

  Jamani mambo gani hayo? Twataka matokeo sisi.Mambo ya kubandikwa yashapitwa na wakati. kitu mtandao bwana

   
 • vianel

  ACHENI KUWANYASANYASA WATOTO WA KITANZANIA KWELI WAMEKAA DARASANI MIAKA SABA HALAFU MUNAWAFUTIA MATOKEO YAO KAMA WALIMU MULIKUWA HAMUWAAMINI BASI MUNGEANDAA WATU MAALUMU WA KUSIMAMIA MITIHANI HIYO KUANZIA PRIMARY MPAKA A-LEVEL ILI KUZUIA TATIZO HILO NAWAOMBA WIZARA MUWAANDAE WATU HATA WANAOMALIZA KIDATO CHA NNE WENYE POINTS 25-28 SIO TU WAENDE KUSOMEA UALIMU TU WENGINE WAKASOMEE NAMNA YA KUSIMAMIA MITIHANI TUMECHOKA KUSIKIA HAYA MAMBO!!!!!!!!!!!!!!!!! HATA MIMI MWENYEWE NIPOTAYARI KUSOMEA KAZI HIYO INGAWA NINAKAZI YANGU-LIBRARIAN. TUMETHUBUTU,TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE KWA LIPI HATA MAJINA HAYAONEKANI KWENYE NET AU MNATAKA TUSEME TUMETHUBUTU, TUMESHINDWA NA SASA TUNAJARIBU INANIUMA SANA HATA POST YA UALIMU MLINIBANIA 2009 NILIKUWA NA POINTS 26 AMBAYO NI NZURI TU MNAWACHUKUWA WATOTO WA WATU WENYE HELA ZAO SS WA MASKINI TUNALIA TUUUU!!!!! MUNGU AWABARIKI NYIE KWA KUWA MKOJUUUUUUUU BY MNGONI WA KWANZA KUWA LIBRARIAN

   
 • RAJABU JUMA

  kwa ujumla serikari ni lazima iwe makini sana na ili kundi la walimu kwa kujua mchango wao mkubwa katika suala la maendeleo katika nchi hii.kwa kuwajali katika mitazamo yote ya ki-uchumi,waswahili wanasema kinyesi si mwiba lakini ukikikanyaga ni lazima uchechemee.YANGU NI HAYO TU!!!!!!!!!!

   
 • Renatus Busanya

  Tunashukru ufaul umeongezeka lakin mfumo wa mitihan tunayo wapa wanafunz haiwajeng sasa lin hisabat ikawa ya kuchagua hapa baraza la mitihan halijafanya lolote bora mrudishe mfumo wa zaman cyo huu.tujarib kutoa mitihan inayo jenga wasomi wa ukwel na c bora wasomi.

   
 • Fr. Mapendo-Chitete

  Kuwajibika ndiyo sehemu ya wajibu wa Waalimu na mfumo mzima wa elimu ya kitanzania. Iweje watoto wadogo hawa wawe na ujuzi wa kuiba mitihani? Kwa kuwa waalimu hawafundishi, maafisa elimu hawakagui mashule iwapasavyo, matokeo yake ni kuandika maswali na majibu ubaoni ili madaftari ya watoto yapendeze kwa alama nzuri.Wanafunzi hawakuiba mitihani, bali waalimu ndiyo waliwaibia wanafunzi mitihani. Hakuna haki ya kuwaadhibu wanafunzi, bali waadhibuni kwanza waalimu husika ndiyo haki itatendeka. Watanzania tuache visingizio, tufanye kazi ipasavyo. Mambo haya yangetokea China, tungekuwa tunazungumza mengine leo!

  Mapendo.

   
 • ALEX MICHAEL

  Matokeo yenyewe yanapatikana kwenye web gani?

   
 • Magabe kesanta

  Hongeleni sana walimu kwa kiasi mlichofikia,Hongela Tanzania b’ze TANZANIA BILA PRIMARY………..no plann

   
 • monica

  even though iam serching since yesterday i didnt find the results.when you will put the result and on which website. please revert me.

   
 • Denis Malle

  Nawapongeza baraza lamtihani Taifa.
  Ila nawashauri waboreshe utendaji kazi,moja ikiwa ni kuwahi kutoa matokeo katika mtandao pili kufikiri kwa kina juu ya wanafunzi waliofutiwa mitihani wapate haki yao kwani siamini hata kidogo kama ni makosa yao.Inawezekana ni makosa ya waliopewa dhamana na Baraza la mtihani kwa kushirikiana na Serikali. Sasa hapo kuna kazi ni kama katika madawa ya kulevya wauzaji wakubwa hawaguswi wanakamatwa watumiaji wadogo wadogo.
  Kwa ujumla Serikali haiko makini kama inavyotakiwa,hivyo kuna haja kubwa ya kufanya marekebisho katika sehemu zote muhimu ili tuende na wakati.
  Tunangojea haraka matokeoya darasa la saba kwa mtandao.
  Kwa leo naomba niishie hapa tu!!!

   
 • Mmbaga

  Nimepata tabu sana tangu jana nilivyosikia kwa masikio yangu taarifa ya habari kwamba watoto 175 wamefutiwa matokeo ya mitihani!!!!! Ni kweli inawezekana kuna sheria ilitungwa kuwa litokeapo hilo hiyo ndiyo adhabu yake. Lakini kwa upande mwingine mtoto wa darasa la saba bado tunamwita mtoto hajafikia hata ile miaka 18 tunayoamini kuwa huyu sasa ni mtu mzima. Mara nyingi mtu mwenye umri chini ya miaka 18, nafikiri si vyema adhabu yake ikawa hiyo, kumfutia mitihani ni kummaliza (fired) ni bora wangemwandhibu hata kwa kurudia mtihani, kumwadhibu (purnishment). Nina imani wengine hata huo mpango wa kuibiwa mtihani hawakuwa wanajua, ni mpango wa wazazi na walimu. Wachukuliwe hatua hao wazazi na walimu, watoto hao chini ya uangalizi mkali wapewe mtihani upya hata kwa gharama za wazazi. KAMA KWELI SHERIA ZINGEKUWA ZINAFUATWA HIVYO KAMA ANAVYOFUATILIWA MWALIMU, MWANAFUNZI NA MZAZI!!! tusingekuwa na msururu wa MAFISADI. Bwana fanyeni mnavyojua ila siku watu watakuja kujua haki zao.

   
 • lutter

  Tusidanganyane wa TZ, Huu mpango wa kufanya majaribio ya kujiunga kidato cha kwanza, maana yake ni kwamba hawana uhakika na watoto waliofaulu kwa sababu Mtihani ulikuwa ni wa kuchagua majibu, hivyo kunawanafunzi wengi wamefaulu kwa kubahatisha tu majibu. Na kwa sababu hiyo mimi sikubaliani na kauli ya kusema eti kwamba ufaulu wa Mtihani umeongezeka kwa mwaka huu, nyie watu wa elimu please fanyeni vitu vya uhakika acheni ubabaishaji, vinginevyo adui ujinga hatuamuondoa TZ!!!!

   
 • kweli watoto hawajatendewa haki, kwamiaka saba yote waliyokaa darasani eti leo hii wanaambiwa kuwa wamefutiwa matokeo inasikikisha sana

   
 • NSEKE

  idadi ya ufaulu iliyoongezeka ni idadi ya ongezeko la wasio jua kusoma na kuandika, serikali haina dhamira ya dhati ya kuinua kiwango cha elimu TZ, kwasababu mwalimu anayenoa kichwa cha mwanafunzi ambaye baadaye tunategemea awe mkuu wa nchi hana motisha. ila wanaangalia wao tu, hivi unadhani hela za nyongeza kwa wabunge hazitoshi kulipa madeni ya walimu? viongozi wetu badilikeni tujenge nchi hii TZ

   
 • Jumanne igenge yohana

  Mimi sioni umaana wa kuyatangaza sasa ikiwa kwenye net hayapo inamaanisha bado tuki kwenye enzi za kipindi kile! Tunataka kila kitu kinachohusu taifa kiwekwe kwenye mtandao siyo mpaka watu waende kwenye mbao kujisomea aibu kwenu baraza la mtihani na wizara ya elimu ,badilikeni zama za hivi zimepitwa na wakati.

   
 • Telesphory

  Ni lazima ufaulu uongezeke kwa sababu hata hesebu ilikuwa ya kuchagua jibu sahihi. Mwanafunzi amefaulu by partial thinking….

   
 • HAFSA SHAHADADI

  Ongera sana walimu kwajuhudi zenu. Wizara acheni mbwembwe mitihani ajachakachuliwa wala nn watoto 2 vipaji.

   
 • VALERIA

  WIZARA YA ELIMU HAPO MMECHEMSHA KABISA!!
  Hamjawatendea haki yao kama watoto kwa kuwafutia matokeo. Hivi mnajua miaka saba ya mahangaiko yao ni muda mrefu kwao? leo hii unamuambia mtoto unamfutia matokeo unategemea nini?na mkiendelea na mpango huo ndo tutakuwa na taifa lenye vijana wavuta bangi,walamba unga, machangudoa n.k kwa sababu umewakatisha tamaa mapema mimi sidhani mtoto wa darasa la saba mwenye umri wamiaka 21-14 afanye udanganyifu mkubwa kiasi hicho. hapo wakulaumiwa ni WALIMU NA WAZAZI wasiopenda kuwajibika.Pia tunaomba matokeo yatolewe kwenye mtandao kwa ni tunahangaika kuyapata.

   
 • Adson baraka

  Hitanzania ni balaa tupu, kila sehemu ni siasa tu,kama matokeo yamechakachuliwa wao walikuwa wapi? hivyo ndivyo tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele.Miaka hamsini ya uhuru oyeeeeee!!!,WACHENI WATOTO WASOME NA SI USANII, ELIMU SI SANAA bana mkubwaaaaaaaaa

   
 • MRS LUCIA GEORGE

  napenda kushauri wizara husika waweke matokeo ya darasa la kwe mtandao cose mwanzo wa elimu zote ni elimu ya msingi saa inakuwaje inaweka njuma jamani tunaomba sana hili mlifanyie kazi

   
 • GEOFREY HILMARY

  JAMANI JAMANI MNATUPELEKA WAPI SASA ACHENI SIASA KWENYE ELIMU HIVI NYINYI MMEKAA KWENYE VIYOYOZI WALIMU WANATESEKA NA UNGA WACHAKI MPAKA MACHO YANAPOFOKA LAKINI LEO MNAPANGA KUWAPA HADHABU BAYA LIPI WALILO FANYA WATOTO WAKIFELI MNAWALAUMU WALIMU WAMEFAULU MNASEA WAMEFANYA UDANGANYIFU AU KWASABABU WATOTO WENU WANASOMA ULAYA. UONIUONEVU USIO NA HURUMA ONGEZENI WALIMU KWAKILA SHULE ONGEZENI MISHAHARA ACHENI KUWACHANGANYA WATOTO WAACHENI WAKASOME. MUNGU AWABALIKI KWANI HUU NI UFALME WANU FANYENI KILA MNALO TAKA KWANI SISI MASKINI HATUNA HAKI ILA UKWELI UTABAKI DAIMA KWANI MLIJENGA SHULE ZAKATA BILA KUWEKA WALIMU KWAKUOFIA TATAKUWA WASOMI NA TUTAJUA KUWA MNATUDHURUMU KWENYE NCHI YETU KUTUFANYA TUWE VIBAKA, WALAUNGA, MACHANGUDOA NA WAOSHA MAGARI YENU YOTE MLIOTUFANYIA TUTALIPWA MBINGUNI asanteni sana.

   
 • makihiyo

  Tumataka matokeo yawekwe kwenye net kwanini mtihani wa hesabu uwe wakuchagua na fourfour mufanye hivyo maana huwezi kuwa na msingi wa nyumba mbovu utegemee kupata nyumba imara asanteni sana

   
 • james lucas

  Tatizo serikali bado hawajajua kuwa tatizo sio kuchakachua tatizo mfumo mbovu wa elimu unaoruhusu utumiaji multiple choice kwa wingi katika mtihan wa darasa la saba hali ambayo inamuwezesha hata asiyejua kusoma afaulu kwani kiwango cha marks chenyewe ni mia moja(100) sawa na marks za masomo mawili tu kwahiyo kuna hatari hata hao waliofaulu ukakuta kiwango kikubwa hawajui kusoma na na hisabati,mfumo uboreshwe kwanza ndio lawama muwafikishie walimu

   
 • sakina

  kweli tunaopendeza necta kwa kazi unayofanya lakini huu mpango sio kabisa kwani muda mrefu japo haizidi siku mbili lakini mpaka sasa hata hamjaingiza matokeo kwenye mtandao ujue kuna ndungu zetu wapo vijijini huwa mpaka waende kata kuangalia wanawaangizia ndungu zao waliokuwa mjini wawaangalizie matokeo kwenye mtandao tunaomba pls wekeni matokeo kwani sasa hivi ni sayansi na tekinolojia

   
 • David john Tuppa

  Mhe.Naibu Waziri wa Elimu pamoja na Wizara yako.Ni aibu mno kwa sababu watoto wamefaulu kinyume na mlivyozoea kutangaza kiwango cha ufaulu kimeshuka;mkabaki kuwalaumu walimu hawajajituma, watoto hawasomi na wazazi hawawakazanii watoto wasome.Malalamiko na maoni ya wadau mengi yaliifanya wizara kubuni mbinu muafaka ili kiwango cha ufaulu kiongezeke. Mwaka huu ikatunga mtihani wa kuchagua, si mbaya kwani hata vyuo na nchi mbalimbali zilizoendelea wanatunga mitihani ya kuchagua.Safari hii watoto wamepewa mtihani wa kuchagua na kwa kuwa wamechoshwa kusimangwa wamefanya vizuri imekuwa nongwa, wanaambiwa wamechakachua.Sasa sijui mlitaka wafeli kama ilivyozoeleka? Mimi siwaelewi kabisa. Watanzania tumeingiza siasa kila mahali. Kuwaadhibu watoto wadogo kwa kwa kuwafutia matokeo ni kuwaonea,hawajatendewa haki.Sera mbovu na siasa za kukamiana ndo mtindo wa wizara yetu.Jifunzeni kwa wengine, ni aibu mno kutangaza watoto zaidi ya 9000 wamefutiwa matokeo? Haiingii akilini.Suala hili serikali lazima iliangalie.Watendaji wizarani ni wabovu na maoni yao ni mabovu yanayowaumiza wengine.

   
 • DAVID DIMOSO

  Jamani huu ni ulimwengu wa sayansi na teknolojia sasa hii tabia ya kubandika matokeo kwenye mbao wakati huu ni msimu wa mvua haina tija yeyote kwa wanajamii. Kwa sasa kuna simu za internet hadi vijijini sasa kwa nini msiweke matokeo kwenye internet? Pia kuweka matokeo kwenye mbao za matangazo huongeza gharama kwa anayeyahitaji kwani matokeo haya hubandikwa katika ya makao ya wilaya sasa je wale wenzangu tunaotoka porini si usumbufu? Wizara ya elimu naomba sana tujifunze kwenda na wakati.

   
 • Michael Bilungo

  Mkongo huu wa taifa una faida gani kama serikali yenyewe inashindwa kuutumia, hata imeshindwa kutangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba 2011. Au mnasemaje wadau, yanapatikana kwenye tovuti gani?

   
 • RAMADHANI RASHID

  Jamani,mimi naamini wizara imeshindwa kuchukua maamuzi ya busara kwani kuwafutia matokeo watoto ni ukiukaji haki za binadamu kwani hao ni watoto wadogo na zaidi walipewa majibu hayo.Hivyo ni vyema kuwachukulia hatua waliohusika iwe kama fundisho .kiukweli wizara ni vyema ikabadili uamuzi huo.

   
 • Salum yubenda

  Ninaishauri wizara ya elimu kutafathari kwa kina jambo hili, shule nyingi zilizoko vijijini hasa ktk mkoa wa singida zilizo na darasa la 1-7, unakuta shule nzima ina walimu 3-4, shule hiyo siku ya mwisho nayo inapewa mtihani ule ule wanaofanya shule Kama ya B. Mkapa iliopo DSM yenye walimu 20-30, je unadhani mtoto anaekula mlenda kila siku atakuwa sawa na yule anaekula samaki? Na je huyo mtoto aliyezoea kula mlenda siku akipata samaki unahisi ni nini nitatokea? Hii ndio maana uchakachuaji wa mitihani hauishi sababu ni wizara ya elimu kutoweka mazingira thabiti ya usawa ktk shule nyingi za vijijini. Na Kama hali hii haitarekebishwa, uchakachuaji mashuleni kamwe hautaishaaaaaaaa

   
 • Sabas F.Rutole

  Kwani kuna sababu gani ya msingi inayozuia matokeo kupatikana kwenye mtandao!!!!Watoto wakiferi lawama kwa walimu,wakifaulu yale yale;sasa mnataka walimu wafanye kipi,mbona haieleweki???!!!!

   
 • Kufanya mtihani tena kwa kigezo cha kupima uwezo wa watoto kama wamefauru kwa uhalali sio shida. Kwanza inadidi tuangalie maadiri ya kazi na nidhamu ya watumishi kwa wale waliosimamia mtihani huo.Ikitokea kwamba mtihani ulichakachuliwa basi walimu ndio wawajibishwe kinidhamu. Lakini watoto wenyewe wapate haki yao kimasomo.

   
 • Safi kwa kiwango cha kufaulu kuongezeka walimu waongeze bidii kufundisha ili taifa lipate manufaa.

   
 • Deus J Chandika

  Jamani sasa yawapasa kuwa makini sana kwani tunakoelekea ni kwenda kuiuwa hii elimu yetu inamaana watoto waliofutiwa matokeo wote walikuwa wameibia mtihani hebu acheni sasa kama mumewafutia mnampango gani nao au ndio muwakalishe majumbani mwao kwani ukiangalia wengi wanatoka katika hali ambayo ni nduni sana.

   
 • Goodluck M Syara

  wapi sasa uhuru wa kujieleza kujitetea kama yanayosemwa haatekelezwi jamani tuwajibike ipasavyo kwenye nafasi tulizopewa

   
 • MANGUSI MANGUSI

  Ongezeko la ufaulu darasa la saba mwaka 2011 siyo kitu cha kujivunia hata kidogo kwani kumetokana na badiliko katiko mfumo wa kujibu maswali.Maswali ya kuchagua majibu yanadumaza elimu moja kwa moja na wanafunzi hawaoni sababu ya kusoma ili wafaulu kwani kwa mfumo huo hata usiposoma swali ukajaza tu jibu uliloamua uwezekano wa kufaulu ni mkubwa sana kuliko wa kufeli.Hakuna elimu ya namna hii duniani ni hapa Tanzania pekee.(
  nawasilisha)

   
 • FRANK

  Jamani serekali tuangalieni tena mfumo wa elimu kwani bila hivyo tutakua tunajenga taifa la wasiokua na elimu ya kweli ila itakua elimu pandikizi isiyokua na manufaa kwa mwanafunzi mwenyewe na mwisho wa siku ziro zitakua zinaongezeka na taifa kudidimia zaidi kielimu

   
 • zeyana

  elimu iko powa kabisa nawasifu tanzania kwa hilo
  hi!kwa wanafunzi wa raskazone tanga

   
 • zeyana

  jamani nimesikia wanafunzi wa ekefod tanga wamefutiwa majibu je ni kweli

   
 

 

Add a comment

required

required

optional