MVUA YAIVURUGA DAR HII NDIO HALI HALISI.

Tunataabika lakini wenzetu wanataabika zaidi…Duh… Wajameni tuhame Mabondeni.

Mhanga wa mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam leo akijiokoa pamoja na Mbwa wake.

Nyumba zikionekana kumezwa na mafuriko ya Mvua.

Mkazi wa eneo la Kigogo jijini Dar akijaribu kujinasua katika mafuriko hayo.

Ni hatari kwa Maisha ya Binadamu kukaa karibu na nyaya za Umeme wakati wa kipindi hiki cha Mvua kali lakini imebidi kufanya hivyo kama picha za Camera ya MO BLOG zinavyoonyesha.

Mhanga  akijiokoa kwa kushikilia bomba la Antena baada ya kuelemewa na nguvu ya maji.

Baadhi ya Wakazi wa Kigogo wakiwa juu ya paa la nyumba yao kwa ajili ya kuokoa maisha yao wakisubiri msaada wa Helikopta zinazozunguka jijini kwa ajili ya kuokoa watu.

Gari la Zimamoto mali ya Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam likiwa limetumbukia kwenye daraja lililoharabika na mvua kubwa iliyonyesha jijini leo.

Wananchi wakitafakari jinsi ya kulinasua gari hilo.

Wakazi wa Kigogo wakionekana kushangaa tukio la kuzama kwa gari la zimamoto.

Mama yangu…eeh Mungu Tunusuru.

Nyumba za Mabondeni zikiwa zimemezwa na maji.

Babu akiokoa baadhi ya Vyombo vyake vilivyokuwa vikipelekwa na Maji.

Foleni na Msongomano wa magari katika Barabara ya Kigogo jijini Dar es Salaam. Wengi wao wakiwa hawana Makazi wala Malazi.

Vyombo vilivyookolewa.

Mwenyezi Mungu awanusuru wanaokaa katika nyumba hii.

Eeeeh…. Mungu tuonyeshe njia kwa maana hatujui la kufanya…!!!

Hali halisi ndio kama hii.

Namshukuru Mungu nimebahatika walau kuokoa mito yangu itanisaidia mbele ya safari.

Wakazi wa Kigogo wakikausha maji yaliyoingia ndani ya nyumba yao.

Hakiachwi kitu hapa… hata kama limeloa, litaenda kukauka mbele kwa mbele: Heka heka za kuhamisha vitu zikiendelea.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional