MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KUMALIZA DARASA LA SABA KENYA YASABABISHA KILIO KATIKA FAMILIA MOJA KIJIJI CHA KETITUI.

Mshituko ulioambatana na majonzi vimekikumba kijiji cha Ketitui kilichopo wilaya ya Kericho baada ya binti mwenye umri wa miaka 14 ambaye alipata alama 145 katika matokeo ya mtihani wake wa kumaliza darasa la saba mwaka huu kuamua kujinyonga.

Binti huyo Mercy Chebet ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya msingi ya Ketitui iliyopo jimbo la Ainamoi, amejinyonga mwenyewe kwa kutomia lesso ndani ya nyumba yao.

Wanakijiji wanasema binti huyo alikwenda shuleni alikokuwa akisoma akiambatana na marafiki zake kwa nia ya kuchukua matokeo yake, lakini alipatwa na mshituko alipokuta kuwa amepata alama chini ya kiwango.

Inaripotiwa kuwa wakiwa katika shamba wakichuma chai binti huyo alimwambia mama yake kuwa amepata alama chini ya kiwango na kumtania kuwa atajinyonga.

Baadae alimuacha mama yake shambani akiendelea kuchuma chain a kuelekea nyumbani ambako alijinyonga.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

1 Comment

 

 

Add a comment

required

required

optional