Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Anne Makinda akitoa wasifu wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum ( Chadema) Regia Mtema wakati wa kutoa heshima za mwisho katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo kufuatia mbunge huyo kufariki Januari 14 mwaka huu kwa ajali ya gari iliyo tokea mkoani pwani.
Mwakilishi wa Familia ya marehemu Bw. Kanute Mtema akitoa maneno ya shukrani kwa serikali, ndugu, Jamaa na Marafiki waliohudhuria wakati wa kuaga mwili wa marehemu Regia Mtema.
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda (kulia), Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bw. Freeman Mbowe (katikati) na Waziri wa Nchi Katika Ofisi ya waziri Mkuu Mh. William Lukuvi (kushoto) wakiwa katika hali ya majonzi.
Mama mzazi wa marehemu Bibi Catherine Haule (katikati) akiwa katika huzni kubwa kufuatia kuondokewa na mwanaye mpendwa Regia Mtema.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Garib Bilal na mkewe wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Regia Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari iliyotokea mkoani Pwani.
Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda akitoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHEDEMA) Bw. Freeman Mbowe akiaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum kupitia tiketi ya chama hicho.
Mh. Lyatonga Mrema akiaga mwili wa marehemu.
Mbunge wa Bumbuli Mh. January Makamba akiuaga mwili wa Regia Mtema.
Mh. Nimrodi Mkono Mbunge wa Musoma Vijijini.
Mbunge wa Viti Maalum Singida Mjini Mh. Diana Chilolo akitoa heshima za mwisho.
Mh. Andrew Chenge.
Mh. Martha Mlata akijifuta machozi kwa uchungu.
Mh. Rita Mlaki akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Regia Mtema.
Mh. Waziri Steveni Wasira akiuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum (CHADEMA) Regia Mtema.
Mbunge wa Iramba Mangaribi Mh. Mwigulu Nchemba akiwa haamini macho yake.
Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHEDEMA) Mzee Mark Bomani akibebwa baada ya kushindwa kujizuia mara tu baada ya kuuona mwili wa marehemu ukiwa ndani ya jeneza.
“Pole sana Mheshimiwa ni Mipango ya Mungu” Ndivyo anavyoonekana kusema Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi (kushoto) akimwambia Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa chama hicho Regia Mtema.



























