MBUNIFU WA MAVAZI ESKADO BIRD KUTUMIA FANI YAKE KWA MAENDELEO YA NCHI KWA UJUMLA.

Na Mwandishi Wetu.

Mbunifu wa mavazi anayekuja juu kwa kasi nchini Doreen Estazia Noni amesema kuwa atatumia aliyojifunza katika mkutano wa Uchumi Duniani kuendeleza fani yake ya ubinifu wa mavazi na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

Noni ambaye anamiliki lebo yake ya Eskado Bird amesema kuwa mkutano huo umemfungua sana katika suala la kimaendeleo na kukuza kipato kutokana na mafundisho yake.

Amesema kuwa katika mkutano huo alishiriki kama mjasiriamali kupitia masuala ya mavazi, aliweza kubadilishana mawazo na kuapata uzoefu mkubwa kutoka kwa wachumi, wafanyabiashara maarufu duniani mbali ya wakuu wa nchi.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na tajiri maarufu duniani Bill Gates walikuwa miongoni mwa watu mashuhuri walioshiriki katika mkutano huo uliofanyika nchini Uswis kuanzia Januari 25 mpaka 29.

 Amesema kwa kuwa yeye ni “Global Shapers”, ameweza kutoa mada mbalimbali ikiwa pamoja na kuzungumza na wanafunzi wa shule ijulikanyo kwa jina la Swiss Alpine katika kipengele cha ujasiriamali.

Amefafanua kuwa aliweza kubadilishana mawazo na wanafunzi hao kuhusiana na nini anachokifanya ikiwa ni pamoja na kuzungumzia lebo yake ya upande wa mavazi ya Eskado Bird hasa kampeni ya mtindo wake ujulikanao kwa jina la What’s Your Freedom? (WYF?) .

Pia aliitambulisha Kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Miracle Films and Studios Limited.

 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional