OFISI YA MKURUGENZI YA SINGIDA YADAIWA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 50 NA SACCOS YA WATUMISHI WA MANISPAA.

Baadhi ya viongozi wa chama cha akiba na mikopo cha wafanyakazi wa manispaa ya Singida. Wa kwanza kulia ni mweka hazina wa manispaa ya Singida Deo na anayefuata ni katibu wa SACCOS ya wafanyakazi wa manispaa ya Singida Richard Kattan.

Kulia ni mweka hazina wa SACCOS ya watumishi wa manispaa ya Singida Agnes Mbuva na kushoto ni Mhasibu Joseph Masele.

Baadhi ya wanachama wa SACCOS ya watumishi wa manispaa ya Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).

Na.Nathaniel Limu

Chama cha akiba na mikopo cha watumishi wa halmashauri ya Manispaa ya Singida (SITCOWS) kinaidai ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa hiyo zaidi ya shilingi  milioni 50.2.

Katibu wa chama hicho Richard Kattani amesema hayo  mjini Singida kwenye  mkutano mkuu wa chama hicho.

Kattani amesema  kuwa fedha  hizo ni  marejesho  ya mikopo ya watumishi mbalimbali wa Manispaa hiyo  ambayo Ofisi ya mkurugenzi ilitakiwa kukata kutoka kwenye mishahara yao.

Hata hivyo amesema licha ya kukata fedha hizo kutoka kwa watumishi hao, Ofisi ya mkurugenzi  huyo aijaingiza kwenye  akaunti  ya chama hicho  cha akiba na mikopo fedha yoyote  katika kipindi cha kuanzia  Juni  mwaka jana hadi Januari mwaka huu.

Amesema  hali hiyo imeathiri  utekelezaji wa majukumu ya chama hicho kutokana na  baadhi ya wanachama wake kunyimwa mikopo  kwa madeni ya  nyuma  wakati  fedha zao zilishakatwa kwenye  mishahara yao na Manispaa kutumia kwa shughuli zake.

Mgeni  rasmi kwenye  mkutano huo  Mrajisi  msaidizi wa vyama vya akiba  na mikopo  mkoa wa Singida Andrew Msafiri, amekitaka chama hicho kuchukua hatua  za kisheria dhidi ya ofisi ya mkurugenzi ili iweze kulipa deni hilo haraka.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional