POLISI WADHIBITI MAANDAMANO YA KUIPINGA SERIKALI YA SENEGAL.

Nchini Senegal, mashirika ya habari yanaripoti kuwa Polisi wa kutuliza ghasia nchini Senegal wamelazimika kutumia mabomu machozi kuwatawanya maelfu ya waandamanaji wanaoipinga serikali ambao walikusanyika katika uwanja mkubwa wa mji mkuu wan chi hiyo wa Dakar.

Waandamanaji hao wanalalamika kuhusu uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini humo kumuidhinisha rais Abdoulaye Wade kuwania urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi huu.

Rais Wade anakusudia kuwania muhula wa tatu ingawa katiba ilibadilishwa muda mfupi baada ya kushika madaraka ya uongozi na kupunguza idadi ya mihula ambayo rais anaweza kuongoza hadi kuwa miwili.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional