Katibu Mkuu wa mfungamano wa kijeshi wa NATO Anders Fogh Rasmussen(Pichani) amesisitiza kwamba jumuiya hiyo itaendelea na operesheni za kijeshi nchini Afghanistan hadi mwaka wa 2014.
Rasmussen ameitoa kauli hiyo mjini Brussels muda mfupi baada ya kuvuma kwa fununu kuwa NATO inapanga kuyaondoa majeshi yake kutoka Afghanistan.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Thomas de Maiziere na Katibu Mkuu Rasmussen wamesema kwamba hapatakuwa na mabadiliko katika mipango ya NATO.
Sababu ya kutokea mkanganyiko ni kauli zilizotolewa na Waziri wa ulinzi wa Marekani Leon Panetta zilizoashiria kwamba huenda Marekani ikazimaliza operesheni za kijeshi mwaka ujao.








