MTOTO SESILIA EDWARD AAGA DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO.

Marehemu Sesilia Edward enzi za Uhai wake.

Mtoto Cesilia Edward amefariki dunia saa tano usiku wa tarehe 08 katika hospitali ya Regency ya hapa jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amelazwa kwa siku mbili kwa ajili ya matibabu.

Marehemu Cesilia alikuwa na umri wa miaka 14 alikuwa na tatizo la moyo na figo kushindwa kufanya kazi na kusababisha tumbo kujaa maji na kuvimba aligundulika na tatizo hilo tangu alipozaliwa.

Kampuni ya Africa media Group wamiliki wa Channel ten Kupitia kipindi mimi na Tanzania ilifanikiwa kumpeleka marehemu Cesilia nchini India kwa matibabu mwaka 2011 mwezi Oktoba lakini hakufanikiwa kupata matibabu (operation) baada ya madaktari kuthibitisha kuwa alikuwa amechelewa kwa matibabu.

Cesilia alikuwa mtoto ya tima na kulelewa na familia ya Bw. Peter Nyarugembe mkazi wa Mbagara kuu ambaye alikuwa akimlea baada ya kukuta akilelewa na dada yake wilayani Kisarawe na alimkuta na tatizo hilo ila kutokana na hali ya uchumi aliyo nayo hakuweza kumsaidia kupona ugonjwa alio nao na kuamua kuomba msaada kwa wasamalia wema kupitia Kipindi cha mimi na Tanzania.

Marehemu alifikishwa hospitali Jumatatu ya tarehe 6 mwezi huu akiwa na hali mbaya iliopelekea kupoteza fahamu na kumbukumbu kila wakati hali iliendelea hivyo mpaka umauli ulipo mkuta Mungua ailaze roho ya marehemu Cesilia mahala pema peponi Amen.

Marehemu Sesilia Edward enzi za Uhai akiwa na Madaktari wa Hospitali ya Regency jijini Dar.

MO BLOG TEAM: Inatoa pole kwa walezi, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu. Tunaomba Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema Peponi Ameen.

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional