WAKAZI WA SINGIDA WATAKIWA KUCHANGIA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone (kushoto) akitembezwa katika maeneo mbalimbali ya hospitali teule ya wilaya ya Singida iliyopo katika kijiji cha Makiungu na mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Maria Borda (katikati). Kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida Pascal Kulwa Mabiti.

Askofu Desderius Rwoma akitoa nasaha zake kwenye hafla ya uzinduzi wa majengo ya hostel na wodi ya akina mama wajawazito katika hospitali teule ya wilaya ya Singida iliyopo Makiungu. (Picha na Nathaniel Limu).

Na.Nathaniel Limu.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Vicent Kone amesema ni fedheha na aibu kubwa kwa mkazi ye yote mkoani Singida kutokuchangia miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi wa zahanati na vituo vya afya katika eneo lake.

 Dkt. Kone amesema hayo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa majengo ya wodi ya wazazi na nyumba ya watumishi katika hospitali teule ya wilaya ya Singida iliyopo katika kijiji cha Makiungu.

Amesema hivi karibuni kumezuka viongozi wapotoshaji wakubwa ambao wanawadanganya wananchi wasitoe mchango wa aina yo yote kuchangia miradi yao ya maendeleo.

Amesema viongozi hao wanadai kuwa jukumu la kuleta maendeleo au kugharamia maendeleo yote ya wananchi ni la seriklai pekee wananchi hawahusiki kabisa.

Mkuuhuyo wa mkoa amesema kama tatizo ni michango kutafunwa na viongozi wasiokuwa waaminifu, kwa nini isitafutwe njia ya kuwabana ikiwemo ya kuwafanyia uchunguzi wa mara kwa mara. Kitendo cha kuzuia watu wasichangie maendeleo yao, kina hasara kubwa mno na anayefanya hivyo, hawatakii mema wakazi wa mkoa wa Singida.

Dk.Kone ametoa wito huo wa wananchi kuchangia maendeleo yao kwenye jimbo la Singida mashariki ambalo mbunge wake Tundu Lissu,amewakataza wananchi wa jimbo hilo kuchangia kabisa miradi yao ya maendeleo ikiwemo chakula cha mchana kwa shule na kwamba kazi yote,itafanywa na serikali iliyoko madarakani.

Kwa upande wake mhashamu Baba Askofu Desderius Rwoma, alitumia fursa hiyo kuiomba serikali iharakishe kulipatia ufumbuzi wa kudumu tatizo la mgomo wa madakari.

 Amesema anaamini madaktari waliogoma kufanya kazi si kwamba ni  maadui  wa wagonjwa au Watanzania kwa ujumla,na wala hawapendi Watanzania wenzao  wafe, hapana wamegoma ili kuishinikiza serikali iwasaidie kuwalipa vizuri waweze kupunguza makali ya ugumu wa maisha uliopo hivi sasa.

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional