SUGU NA RUGE SASA MAMBO SHWAAAAAAARI.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba  wakipeana mikono leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa  tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Huku wapatanisha wa mgogoro huo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi (kushoto) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (kulia) wakishuhudia.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi  akiongea na waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya  Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo ni  Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.

Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba (kulia) akimsikiliza Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliotokana na sababu za kimuziki uliodumu kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (kushoto) akimsikiliza Mkurugenzi wa Clouds Media Rugemalila Mutahaba wakati akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam juu ya  mikakati ya kufanya kazi kwa pamoja mara baada ya kumalizika kwa mgogoro baina yao uliodumu  kwa muda wa miaka miwili. Wapatanishi wa mgogoro huo ni  Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu. (Picha na Anna Nkinda-Maelezo).

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

2 Comments

  • Anonymous

    Hongereni sana kwa kuwapatanisha hao watu.Lakini hapo ni somo kubwa sana kwa Media nzima ya Clouds kwani inapenda sana kubania baadhi ya wasanii.

     
  • Anonymous

    Ni jambo jema watu kupatana lakini tunahitaji kuona matokeo halisi ya mapatano hayo kwa kazi za wasanii kufanyiwa haki na kampuni ya clouds media,kwani tunafahamu jinsi gani ni wanyonyaji waliovaa sura za msaada.

     
 

 

Add a comment

required

required

optional