ALLAN LUCKY a.k.a SKONGA NA HAIKA SAMWELI HATIMAYE WAMEKUWA MWILI MMOJA.

Gari lililombeba Bibi Harusi likiwasili ukumbini.

Maids na Bwana Harusi wakiwasili ukumbini tayari kwa ibada ya ndoa.

Maids katika pozi.

Bwana Harusi na mpambe wake wakiongozwa na warembo kuingia ukumbi tayari kwa ibada ya ndoa.

Bwana Harusi na mpambe wake wakisubiri kuwasili kwa Bibi Harusi.

Bibi Harusi Haika Samwel akishuka kwenye gari.

Bibi Harusi Haika Samweli akisindikizwa na Mama yake mzazi kuingia ukumbini.

Bwana Harusi akitoa tabasamu bashasha kwa mkewe baada ya kuwasili ukumbini.

Maharusi na wapambe wao wakiwa kwenye ibada ya ndoa.

Bw. Mnyavano kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kinondoni akizungumza wakati wa kufungisha ndoa.

Bwana Harusi Allan Lucky Komba akila kiapo cha ndoa.

Bibi Harusi Haika Samweli akila kiapo cha ndoa.

Put a ring on it Allan.…Bwana Harusi akimvisha pete mkewe.

Bibi Harusi naye akifanya vivyo hivyo kwa mumewe.

You may now kiss the bride….

Duuuuh Siamini kama amekuwa wangu…..!!! Maharusi wakitafakari jambo.

Bwana harusi akianguka saini.

Bibi harusi naye akianguka wino kwenye gamba.

Mpambe wa Bwana Harusi Banana Zoro akitia wino.

Mpambe wa Bibi Harusi naye akifanya vivyo hivyo.

Ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria ibada ya ndoa.

Bwana na Bibi Allan Lucky Komba wakipokea hati ya ndoa.

Bibi Harusi akiwa katika picha ya pamoja na wazazi wa Bwana Harusi.

Wazazi wa Bibi Harusi (kushoto) pamoja na  Mama Mkwe.

Familia Bwana Harusi na Maharusi.

Sasa ni mwili mmoja.

Maids wakila pozi na Bwana harusi.

Bwana na Bibi Allan Lucky na Maids wao.

Maids wakiingia ukumbini kwa style ya aina yake.

Bwana na Bibi Allan Lucky Komba wakiingia ukumbini na nyuso za furaha.

Maua ya Rose yalitawala ukumbi mzima kuwashangilia maharusi.

Shangwe, nderemo na vifijo vilitawala ukumbini.

Swaga za Kingoni.

Maharusi na wapambe wao wakiwa meza kuu.

Mr. & Mrs Allan Lucky wakipozi meza kuu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Harusi Bw. Mussa Kondo (kushoto) akitambulisha kamati yake.

Bwana Harusi akitoa utambulisho wa familia yake.

Kaka wa Bwana harusi akisalimia wageni waalikwa.

Mrs. Allan akitoa utambulisho kwa familia yake.

Mama mzazi wa Bibi Harusi akisalimia wageni waalikwa.

Ninapotaka mimi ni hapo tu ninapotaka mimi ni hapo…..wangoni ni nomaaa.

Wachaga nao hawakubaki nyuma.

It’s time to pop up the Champagne.

Wedding Planner Mage akifurahia kufunguka kwa Champagne yake.

Wafanyakazi wa EATV wakitoast na maharusi.

Ukawadia muda wa kukata Cake.

Mr. & Mrs. Allan Lucky wakikata Cake.

Wakilishana Cake.

Bwana Harusi akikabidhi Cake kwa wakwe zake kama Asante.

Bibi Harusi naye alifanya vivyo hivyo.

Wakati wa maakuli uliwadia.

Naomba kuwakilisha : Operation Manager wa MO BLOG Zainul Ali Mzige (kushoto) na mrembo Irene Mosha wakijichana kwa mnyopnyop katika harusi hiyo. 

Warembo walivunja makabati ni noumaaa.

Mkuu wa vipindi EATV Lydia (katikati) wakitazama matukio wakati wa sherehe ya harusi ya SKONGA.

Pichani Juu na Chini ni Vijana wa EATV and Radio waliojumuika na Allan Lucky kusheherekea pamoja.

Mtangazaji wa East Africa Radio kipindi cha Super Mix Michael Baruti (kushoto) akiwa na rafiki yake.

Lotus katika pozi.

Vijana fwateni nyayo zangu……Bwana harusi katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao ni mabachelors.

Kwaito zilichezeka kwa sana.

Sebastian wa EATV na Radio wakitoa shoo ya kufa mtu na mfanyakazi mwenzake kwa maharusi.

Hapo chacha twende kazi….Maids nao hawavumi lakini  wamo.

MC wa Shughuli Patrick Nyembela alisahau kazi yake kidogo na kujumuika na maharusi kulisakata rumba.

Mzuka umewakolea Vijana wa EATV, huku wengine wakiona viatu vizito na kuamua kuvua kabisa.

Marygoreth akiwa na Bwana harusi na Bestman. Unaweza kumtembelea Marygoreth humu http://marygorethrichard.blogspot.com/

Twist limekolea hapo mpaka chini…..

MC Patrick Nyembela na wafanyakazi wenzake wakitoa mkono wa pongezi kwa maharusi.

Wafanyakazi wa EATV wakiwa na HP wao Lydia.

Wageni waalikwa.

Stay tuned for Nirvana Show on EATV, Fashion Police.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandilizi ya Harusi ya Allan Lucky Bw. Mussa Kondo akizungumza machache wakati wa kukabidhi zawadi ya kamati kwa maharusi.

Kamati ya maandalizi na maharusi.

Irene Moshi katika picha na maharusi.

Single Ladies wakigombania Ua lililorushwa na Bibi Harusi.

 she is the Lucky Girl to catch it.

Shangwe zote hizo zilisababishwa na mtu mzima DJ KIM a.k.a The Big Man Kim.


 
 
 

About the author

More posts by

 

15 Comments

 

 

Add a comment

required

required

optional