Naibu waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu maadhimisho ya 24 ya wiki ya maji ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Iringa kuanzia tarehe 16-22 mwezi huu . Wadhamini wa Maadhimisho hayo ni Kampuni ya Bia ya Serengeti na ITV na Redio One huku Kaulimbiu ikiwa ni Maji na Usalama wa Chakula.
Naibu waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi huduma za maji vijijini ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya maandalizi ya maadhimisho ya 24 ya wiki ya maji Mhandisi Amani Mafuru mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari huku Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhandisi Christopher Sayi akifuatilia kwa ukaribu mazungumzo hayo. Maadhimisho hayo yatafanyika kitaifa mkoani Iringa kuanzia tarehe 16-22 mwezi huu huku Kaulimbiu ikiwa ni Maji na Usalama wa Chakula.(Picha na Anna Nkinda-MAELEZO).









