MH. TUNDU LISSU APANGUA TUHUMA DHIDI YAKE KATIKA KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UBUNGE ILIYOTIA FORA MKOANI SINGIDA KWA KUHUDHURIWA NA WATU WENGI.

Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu akipongezwa na wanachama wa CHADEMA, mara baada ya kuwasilisha pingamizi za kupinga kesi iliyofunguliwa ya kutaka kutegua ushindi wake wa ubunge.

Mawakili wa serikali Vicent Tango (mbele) kutoka mkoa wa Mbeya akifuatiwa na ni wakili kutoka Arusha Ramadhan Mzalah na wa mwisho ni Abdalah Chavula kutoka Moshi.

Wakili wa waomba maombi ya kutegua ushindi wa Mh. Tundu Lissu Godfrey Wasonga.

Muuza maji Singida mjini maarufu kwa jina la CHADEMA One, ambaye aliacha kuuza maji mjini na kwenda kusikiliza kesi ya Tundu Lissu. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Na. Nathaniel Limu

Mabishano makali ya kisheria yametawala wakati kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge jimbo la Singida mashariki Mh. Tundu Lissu kupitia tiketi ya CHADEMA.

Kesi hiyo ambayo imevunja rekodi kwa kuhudhuriwa na wasilikizaji wengi mno, inasikilizwa na jaji Moses Mzuna wa mahakama kuu kutoka Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Washitakiwa katika kesi hiyo ya uchaguzi ambayo ni ya kwanza kusilizwa mkoani Singida, ni Tundu Lisu, mwanasheria mkuu wa serikali na  msimamizi wa uchaguzi jimbo la Singida Mashariki.

Tundu Lissu anajitetea yeye mwenyewe, mwanasheria mkuu wa serikali na msimamizi wa uchaguzi, wao wanatetewa na mawakili wa serikali Vicent Tango kutoka Mbeya, Ramadhani Mzalau kutoka Arusha na Abdala Chavula wa Moshi.

Upande wa waomba maombi ya kutegua ushindi wa Tundu ambao ni Shaban Itambu na Pascali,n wanatetewa na wakili msomi kutoka Dodoma Godfrey Wasonga.

Katika hoja yake ya kwanza Mh. Tundu amesema maombi yaliyowasilishwa mahakamani, sio maombi halali kisheria kwa sababu ada iliyowekwa na sheria kwa ajili ya kufungulia madai hayo haijalipwa.

Amesema ada iliyowekwa kisheria kwa mujibu wa sheria namba 8 (1) ya kanuni ya uendeshaji kesi ya uchaguzi ya 2010, ni shilingi laki mbili, lakini waombaji wamelipa shilingi 12,500/= tu, kupitia stakabadhi No. 40696065 ya Novemba 30 mwaka 2010.

“Hoja hii peke yake inatosha kufutilia mbali maombii ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Singida Mashariki na kuwaamuru walete maombi haya, kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi hii” alisema Tundu.

Katika hoja yake ya pili, Tundu amesema tuhuma zilizotolewa na waleta maombi katika vifungu kuanzia cha saba hadi 18, sio halali kisheria.

Akifafanua, alisema tuhuma hizo zimeandikwa katika lugha ya jumla jumla ambazo sio rahisi kujibiwa kisheria.

Amesema maelezo yanatakiwa yawe yanajitosheleza kikamilifu yasiwe maelezo ya jumla jumla.

Baadhi ya tuhuma ambazo Tundu amesema ni za jumla jumla ni pamoja na hoja inayodaiwa kuwa alitumia ukabila na udini wakati wa kampeni.

Tundu amesema lakini hakuna mahali kumeonyeshwa ni wapi alitamka maneno hayo wala hapajatajwa ni matamshi gani.

Aidha katika tuhuma ya nane inayodai Tundu kutoa mafunzo kwa wanachama 140 wa CHADEMA na vyama vingine isipokuwa CCM juu ya namna ya kuvuruga uchaguzi.

Alisema wapewa mafunzo hao 140, hawajatajwa majina na vyama vyao na waleta maombi ya kupinga ushindi wake.

Hoja ya 12, ambayo tuhuma imetolewa kuwa mawakala wa Tundu walitumia nguvu na amri katika vituo kadhaa kwa wapiga kura ambao uoni wao sio mzuri kwa lengo la kutaka wampigie Tundu.

Tundu amesema tuhuma hiyo haijaainisha ni nguvu za aina gani zilitumika, ngumi au mapanga. 

Haijataja vituo vya kupigia kura wala majina ya watu wenye uoni hafifu au kadi zao za kupigia kura.

Hizo ni baadhi ya tuhuma alizozipangua Mh. Tundu Lissu.

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional