Mkuu wa Sera za Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya anafanya ziara nchini Burma ikiwa ni sehemu ya Umoja huo kuunga mkono mabadiliko ya kisiasa ya hivi karibuni nchini humo.
Mkuu huyo Catherine Ashton (pichani) amesema Umoja wa Ulaya unakusudia kufungua ofisi mpya ya kibalozi katika mji wa Rangoon.
Bibi Ashton amekutana na Kiongozi wa Kidemokrasia nchini humo Aung San Suu Kyi na pia anatarajia kufanya mazungumzo na mawaziri wa serikali inayoungwa mkono na jeshi.
Mapema wiki hii Umoja wa Ulaya ulikubali kusitisha vikwazo dhidi ya Burma kwa kipindi cha mwaka mmoja ikiwa ni kutambua mabadiliko ya kihistoria nchini humo.
Hata hivyo kikwazo cha mauzo ya silaha bado kinaendelea.








