Katibu Mkuu wa Hazina Bw. Ramadhani Khijjah (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero wakitia saini mkataba wa makubaliano ya mkopo wa shilingi bilioni 354.56 wenye lengo la boresha sekta ya barabara nchini. Mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Oktoba 2012 na kazi hiyo kukamilika Machi 2017.
Bw. Ramadhani Khijja na Tonia Kandiero wakibadilisha mkataba huo baada ya kutiana saini leo jijini dae es Salaam.
Na.MO BLOG TEAM
Serikali ya Jamhuri ya Tanzania imetiliana saini mkataba wa makubaliano ya mkopo na Mfuko wa Maendeleo wa Afrika wenye thamani ya shilingi bilioni 354.56 ikiwa ni Awamu ya Pili ya Mradi wa Kusaidia Sekta ya Barabara hapa nchini.
Katika kutiliana saini mkataba huo serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Hazina Bw. Ramadhani Khijjah wakati Benki ya Maendeleo ya Afrika iliwakilishwa na Mwakilishi Mkazi Tonia Kandiero.
Madhumuni ya Mradi huo ni kuboresha mfumo wa miundo mbinu ya usafirishaji kwa njia ya barabara kwa nia ya kupunguza gharama za matengenezo ya barabara, gharama za vyombo vya usafirishaji na muda wa kusafiri.
Mradi huo utatekelezwa katika mikoa ya Dodoma, Manyara and Ruvuma katika kipindi cha miaka mitano (5) kuanzia 2012 hadi 2017.









