SERENA NA VENUS WILLIAMS WATUPWA NJE “FRENCH OPEN”.

Venus akiwa bado anapambana katika mzunguko wa pili wa “French Open” ambao alifungwa kwa siti 6-2, 6-3 na Agnieszka kutoka Poland. 

Serena Wiliams akiwa ameishiwa nguvu baada ya kuona maji ya shingo, baada ya kupoteza matumaini ya ushindi dhidi ya Razzona juzi katika mzunguko wa kwanza.

Ndugu wawili Serena na Venus Wiliams wametupwa nje kwenye mashindano ya Tenesi “FRENCH OPEN”  yanayoendelea mjini Paris, Ufaransa.

Baada ya Venus kutolewa juzi katika mzunguko wa kwanza, Venus nae jana ameshindwa kuipeperusha vyema bendera ya familia hiyo ya kimarekani baada ya kufungwa na  Agnieszka Radwanska  wa Poland kwa seti 6-2, 6-3.

Akiwa bado anasikitikia matokeo ya nduguye Serena  aliyetolewa mzunguko wa kwanza na Virginie Razzano wa Ufaransa baada ya kucheza seti 3.

“ilikuwa ngumu sana kwangu sababu matumaini yangu yote yalikuwa kwa Serena katika mashindano haya, nilitaka sana ashinde. Amekuwa akicheza vizuri sana siku zote, lakini huo ndio mchezo” alisema Venus Williams

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional