HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA IMEANZISHA USHIRIKIANO NA JIJI LA KOKKOLA LA NCHINI FINLAND.

Mstaiki Meya wa Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa akipata maelezo kutoka kwa Bw.Ronny Snellman wa Kampuni ya utengenezaji wa nyama ya Snellman ilioko nchini Finland  alipotembelea machinjio yao yaliyo katika mji wa Jakobstad. Halmashauri ya manispaa ya Ilala imeanzisha ushirikia na jiji la Kokkola la nchini Finland.Uhusiano huu utasaidia kuleta maendeleo katika Manispaa ya Ilala kwenye maeneo ya utawala bora, biashara ,usindikaji matunda, nyama na maziwa, nishati mbadala, utengenezaji wa boti na usafi wa mji. Ujumbe wa mstahiki Meya unajumuisha Mhe.Godwin Mbaga ambaye anaratibu ushirikiano huo katika ofisi ya Meya, Bw.Sigfid Valentine ambaye ni mkuu wa Idara ya uchumi na mipango wa Halmashari na Mratibu wa ushirikiano, Bi.Tabu Shaibu Afisa uhusiano,A fisa Mifugo Juma, Afisa biashara Nicas na Afisa Teknohama Matilda.

Wengine katika picha ni Afisa biashara Bw. Nicas na Afisa mifugo Bw. Juma mwengine ni Bw. Stefan Jungell wa kampuni ya Kosek amabyo ni kampuni ya maendeleo ya jiji la Kokkola.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional