Madam Ritha akipokea mtoto kutoka mshiriki huyu aliyekuja nae katika shindano hilo kabla ya kuanza ya kuanza kuimba.
Mmoja wa washiriki akionyesha kipaji chake mbele ya majaji wa EBSS 2012 (hawapo pichani).
Mmoja wa washiriki akipongezwa na Ndugu yake baada ya kuibuka mshindi.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012 Awaichi Mawalla akichangia damu ikiwa ni maadhimisho ya siku ya wachangia damu Duniani.
Na.Mwandishi wetu
Pazia la shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS) kwa mkoa wa Dodoma limefungwa rasmi huku vipaji kibao vikiwa vimejitokeza na kuwavutia majaji.
Kilichovutia zaidi ni washiriki wa miaka 16 ambao wameonekana kuimba vema na kuwa kivutio hata kwa washiriki wenzao waliofurika katika ukumbi wa Royal Village.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Benchmark Production inayoandaa shindano hilo Ritha Paulsen amesema kuwa amevutiwa na wingi wa washiriki mkoani Dodoma hasa idadi ya washiriki wasichana pia.
Amesema kuwa ikiwa ni mara ya kwanza kuruhusu washiriki wa miaka 16 kuingia katika usaili wa EBSS 2012 ameshuhudia hazina kubwa ya vipaji vya washiriki wa umri huo.
Katika usaili huo kulikuwa na washiriki wa aina mbalimbali wakiwamo wanafunzi, wafanyabiashara ndogondogo, vijana wa mitaani na wadau wengineo wa muziki.
Kwa kuthamini umuhimu wa akina mama na watoto mshiriki aliefika kuonesha kipaji chake katika ukumbi huo alipewa nafasi ya kuimba ili aweze kuwahi kuondoka.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Zantel ambao ni wadhamini wakuu wa EBSS 2012 Awaichi Mawalla mbali na kuvutiwa na ushiriki wa vijana waliojitokeza pia amehamasisha upimaji wa damu kwa kuchangia damu kwa kituo cha damu mkoani Dodoma.
“ Kwa kupitia EBSS 2012 tunataka kuwafikia vijana sio tu katika muziki bali pia hata katika kuhamasisha masuala mbalimbali yahusuyo jamii kama vile hili la kuchangia damu na mengineo” alisema Awaichi.
Washindi watakaopatikana watatangazwa baadae katika vyombo vya habari.
Baada ya Dodoma kwa sasa inafuata Zanzibar Ijumaa ijayo katika eneo la Ngome Kongwe.












at 5:25 am
Dodoma ni Mji Mkuu wa Tanzania. Nafurahi sana kwamba wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi, hivyo kuupa hadhi ya juu mji huo. Na si kujitokeza tu, bali kwa vipaji walivyonavyo. Wenyeji wa Mkoa huo, kiasili huwa wana sauti tamu sana. Wakikuimbia nyimbo zao unapata burdani safi sana! Hasa nyimbo za kigogo na marimba. Utapenda!!!! Sasa Madm Rita kazi kwako. Hongera sana!