MILLARD AYO AFUNGUKA KWA MO BLOG JUU YA AJALI MBAYA ILIYOWAHI KUMTOKEA MAISHANI.

-PIA AMZUNGUMZIA JINSI ALIVYOONDOKA RADIO ONE NA UHUSIANO WAKE NA MKURUGENZI WA ITV/RADIO ONE.

SEHEMU YA KWANZA.

Kama ilivyo kawaida kwa wataalamu wa masuala ya habari na kijamii wa mtandao wa MO BLOG unaotisha kwa sasa, Mhariri Mkuu wa Mtandao huo Lemmy Hipolite na Meneja Mipango Zainul Mzige ‘hamad’ uso kwa uso na mtangazaji maarufu wa Radio na Televisheni hapa nchini Millard Ayo.

LEMMY: Haya ndugu yangu za masiku hatuonani ila mimi nakuona tu kwenye luninga.

AYO:  Aiyaa….! Wakuu ni aje ni kitambo kimepita hatujaonana ila mimi niko poa tu nakaza buti.

ZAINUL: Usiende mbali tunajua uko bize lakini hebu kaa kitako uzungumze na mhariri wangu kuhusu mawili matatu watu wasio yajua kuhusu wewe.

MO BLOG: Nini kimeshawahi kukutokea maishani ambacho huwezi kukisahau na wasikilizaji na watazamaji wako hawakifahamu.

MILLARD AYO: Nilishawahi kupata ajali mbaya kiasi kwamba watu wengi wasingekuwa wananifahamu hivi leo. Ni ajali ambayo iliondoka na rafiki zangu wanne.

MO BLOG: Pole sana na tuna muomba Mwenyezi Mungu Mwenye Rehema Awarehemu.

MILLARD AYO: Amina.

Tulikuwa tunasafiri na basi katika safari za kishule, tulikuwa 60 hivi kwenye basi tukapata ajali ‘Ngongoro crater’ bonde la ufa sehemu inaitwa ‘Malanjo Cross’ ni sehemu hatari sana, yaani tuliingia bondeni, yaani sidhani kama leo ningekuwa hai.

MO BLOG: Hebu Millard tufafanulie zaidi tukio hilo la ajali lilikuaje..?

MILLARD AYO:  Yaani sina la kusema ila kama Mungu asingependa mimi nisingekuwepo duniani, lakini kwa sababu alipenda, ndio maana nipo, hata hili kovu katika kichwa upande wa kushoto lipo. Hapa iliingia chuma, unajua mabasi ya zamani yalikuwa na chuma, sasa ile chuma ilikatika wakati basi likijipiga kwenye mawe kama unavyojua kule ni crater.

Kwa kweli ninachokumbuka ni kuwa gari lilipotulia watu walikuwa wakilia na damu zinatiririka na mimi nilikuwa nimebanwa katika hiyo chuma na nilipotolewa sikukumbuka tena nini kiliendelea.

Ilikuwa mbaya sana kwa sababu lile basi lilikuwa likibiringika kama chupa, hivyo watu wanatupwa  madirishani na kisha gari linawalalia ndio mazingira watu walivyopoteza maisha.

OMG…!!!

 MO BLOG:  Kitu kingine ambacho MO BLOG ingependa kufahamu ni kuondoka kwako ITV, fununu zinasema kuwa ulikuwa ni mtiti, ni ya kweli haya?

 MILLARD AYO: Ningependa watu wakifahamu ni kuwa mimi sina ugomvi na ITV wala sikuondoka kwa ugomvi.

Kwanza kufanya kwangu kazi ITV naamini Mungu alikuwa anaona na alipanga ndio maana hata hivi sasa kuna uwezekano kuwa nafasi nyingine nilizo nazo maishani kwangu nisingezipata, pengine hata ‘Clouds’ wasingeniona na wasingenifuata.

ITV ndio ilimtambulisha Millard Ayo.

ITV niliondoka vizuri ndio maana nitawaheshimu na nitazidi kuwatangaza vizuri popote nitakapokwenda.

Kwa sasa hapa ‘Clouds Radio’ nafanya show yangu ya ‘Amplifaya’ ambayo ina sehemu inayohusisha Blogs, Facebook na Twitter.

Katika kipengele hicho nasoma sana habari zao wanazo zi’tweet’ na nasema nimezitoa ITV.

 MO BLOG: Zungumzia mahusiano yako na viongozi wa ITV na wafanyakazi wake.

MILLARD AYO: Nasema ukweli kuwa sina kinyongo na Mkurugenzi Mkuu wa ITV Joyce Mhaville tena namwambia asante sana kwa kunilea, sina matatizo na waliokuwa wafanyakazi wenzangi wa ITV na Radio One na tunaendelea kuwasiliana kama kawaida na nawaambia tuko pamoja na nawapenda sana.

Wengine tunakutana na tunakuwa ‘good times’ pamoja na bado nitaendelea kuwaheshimu kote nilikotoka ikiwemo ITV, WAPO RADIO na TVZ, hata kama kuna mapungufu, hakuna sehemu isiyokuwa na mapungufu.

Wasikilizaji wa ‘Amplifaya’ msisite kusikiza kipindi hiki kwa sababu kila unachokipenda utakipata humu na pia mimi kama Millard Ayo nasema “MO BLOG MO BENEFIT”.

Msomaji wa Blog hii usikose SEHEMU YA PILI ya mahijiano ya MO BLOG na MILLARD AYO ambapo amezungumzia maisha yake ya kimapenzi na suala tata linalovuma hivi sasa la ‘FREEMASON’.

Usipoperuz mtandao wa www. Dewjiblog.com utaachwa tutani…!

Mahojiano na Uandishi: Lemmy Hipolite.
Msimamizi: Zainul Mzige.

Millard Ayo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mhariri Mkuu wa MO BLOG Lemmy Hipolite (kushoto) na Assistant Operation Manager

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

17 Comments

  • pole sana bwana Millard na ahsante Mo blog kwa nice interview!

     
  • TerryKrikuk

    It is a very moving traumatic story Millard, Big up for the good job you are doing boy.

     
  • robert mgangala

    pole xana millard ayo! na pia endelea kukaza buti we mkali bana!!

     
  • Kama kuna kitu nilikuwa natamani ni millard Ayo kuhojiwa siku moja. I love u so much ma young na habari zako, pole na yaliyokukuta ni mtiririko tu wa maisha. Ahsante mwnahabari kwa habari zaiidi naendelea kusubiri sehemu yapili.
    All di best wandugu.

     
  • Mimi ni mwanamama mtumzima, nikimpenda sana huyu mwanangu Millard utangazaji wake wakati yuko ITV, hata kama niko mbali husogelea karibu na TV khassa pale anapotangaza Taarifa ya Habari, kwani ni kijana mtulivu, alikua akijiamini anaposoma habari na kwa kweli alinifanya nipende kuangalia taaria ya habari kutoka ITV na zaidi nikimpenda kwa utulivu wake wakati akisoma, tangu aondoke kwa kweli nami nimeihama!. Nashangaa kwa kweli kukubali kumuachia kijana kama huyu aondoke ingawa nisingependa kujua kwanini, lakini lazima kutakua na sababu. Mwanangu, endelea kukaza buti, Mungu atakujaalia uwe na maisha mazuri huko uliko sasa na ufanikiwe katika ndoto zako Millard! Amina, kwani maisha ni milima, kuna kupanda, kushuka na hatimae kufika, utafika mwanangu!!

     
  • Sasa Milard Ayo, kama unatuhakikishia kuwa umeondoka vizuri sehemu yako ya kazi ya zamani,unasema pia utawatangaza vizuri kokote hizo ni DALILI NZURI KUWA huna kinyongo na mtu wala nia mbaya dhidi ya yeyote!, ila hizo TWEET kutoka sehemu yako ya awali ya kazi ndio vipi tena?

     
  • Good good…tiririka second interview utuletee shemeji yetu… usije ukawa una amplify za watu wako yuko wapi??

     
  • goodchance lyimo

    BRO POLE XANA KWA AJALI BUT YOU SHOULD REAL THANK GOD FOR HE HAS A REASON FOR YOU TO LIVE. I LIKE DA APPRECIATION AND ACKNOWLDGEMENT YOU MADE CONCERN ITV UMEONESHA UUNGWANA NA WEMA KWAO. BG UP XANA KAZA BUTI KIJANA MWENZETU.

     
  • julius emily

    ongera sana kwa kushukuru kwako kwa kutoka itv sababu watu wengi huwa wana ondoka maeneo yao ya kazi kwa mizengwe ,ugonvi na vitu kama hivyo .
    yes kaz bro hapo clouds

     
  • ally sabu

    big up ma young braza, wewe mkali sn….

     
  • Kaka pole sana na mungu akuwezeshe kufikia malengo yako kaza butu kaka yangu maana maisha ya sasa si kupoteza muda hata kidogo.

     
  • JOYCE

    M I LL AR D A Y O. UPO JUU SANA. FIRST TIME KUKUONA UKITANGANGA HABARI. I WAS LIKE WOOOOOOW KIJANA ANATANGAZA VIZURI SANA. USHAURI TAFUTA KIPINDI AMBACHO UNAONEKANA LIVE.. UTAJITANGAZA ZAIDI KULIKO REDIO. UKO PRESENTABLE NA UNAJUA UNAFANYA NINI. AM OUT

     
  • igalla

    Maisha ni historia pole sana ndg,kazi yako inaonekana,USILALE

     
  • frank

    mimi ni miongoni mwa mapresenter machipukizi ndani ya bongo lakini kiukweli uwa namzimia sana millard anapo kuwa katika amplifaya ndani ya clouds big up kwako kaka kaza buti na sisi kunawatazama nyinyi kaka allaaaaaaaah

     
  • daa pole sana kaka mungu ndiye mpanga wa yote ndiyo maana alikuepusha hadi leo huko hai na unaendelea kuwaelimisha watanzania big up kaka