WANAFUNZI WATANO WAFARIKI NCHINI UGANDA BAADA YA MABWENI KUUNGUA MOTO.

Wanafunzi watano wameteketea kwa kuungua kwa moto nchini Uganda baada ya moto kuunguza mabweni mawili ya Leos Junior Academy katika manispaa ya Masaka.

Wanafunzi wote waliofariki ni wa elimu ya msingi ambao wameungua hadi kutotambulika, na miili yao imepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Masaka.

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kusini Simon Peter Wafana amesema tayari polisi nchini humo imeanzisha uchunguzi wa chanzo cha moto huo.

Hii ni mara ya pili moto kuzuka katika shule hiyo katika kipindi cha miaka miwili.

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional