Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania na kuhudhuriwa na wadau wake mbalimbali wakiwemo wakuu wa wilaya.
Baadhi ya wadau mbali mbali wa mawasiliano wa mkoa wa Singida wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinatolewa kwenye semina ya mawasiliano.
Mkurugenzi wa manispaa ya Singida Mathias Mwangu akichangia mada kwenye semina ya wadau wa masiliano mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone (wa tatu kutoka kushoto,walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa mawasiliano na viongozi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA). Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Innocent Mungy na anayefuata ni Kaimu Meneja (TCRA) Elly Benard. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa wilaya ya Iramba Ismael na anayefuata ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amewatahadharisha wananchi wenye lengo la kuvuruga zoezi la kuratibu maoni ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa, wakithubutu watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Akifungua semina ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania iliyofanyika mjini Singida, Dkt. Kone amesema kwa vyo vyote vurugu ya aina yoyote, zinaweza kusababisha wananchi wakose uhuru wa kutoa maoni yao ambayo ni muhimu katika kupata katiba itakayokidhi matarajio ya wananchi.
Katika hatua nyingine, Dkt. Kone amesema wananchi wengi zaidi wanahitaji kuifahamu mamalaka ya mawasiliano Tanzania na majukumu yake ili waitumie.
Kuhusu wanasemina, Dkt. Kone amewataka kufikisha kwa wananchi elimu watakayoipata kwa vile wao hawakupata nafasi ya kuhudhuria semina hiyo.
Awali Kaimu Meneja kanda ya kati wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania Elly Benard, alitaja baadhi ya mada za semina hiyo, kuwa ni pamoja na majukumu ya mamalaka ya mawasiiano Tanzania (TCRA), mfumo mpya wa utangazaji wa digital na haki na wajibu wa wateja wa huduma za mawasiliano.











