WATU 18 WASHIKILIWA NA POLISI SINGIDA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM.

Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Vicent Sinzumwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha)  juu ya mauaji yaliyofanywa na wafuasi wa CHADEMA. (Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Jeshi la polisi mkoa wa Singida linawashikilia wakazi 18 wa kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi kwa tuhuma ya kumuua mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM) Yohana Mpinga (30) baada ya kumpiga kwa kutumia silaha za jadi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Vicent Sinzumwa amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea Julai 14 katika kijiji cha Ndago.

Amesema siku ya tukio, Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kilikuwa na kibali halali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha Ndago na mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa mbunge wa jimbo la Ubongo jijini Dar-es-salaam.

Sinzumwa amesema mara baada ya CHADEMA kuanza mkutano huo, viongozi wake walianza kuporomosha mvua ya kashifa mbalimbali dhidi ya mbune wa jimbo hilo Mwingullu Nchemba, kitendo ambacho kiliudhi baadhi ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.

Kamanda huyo amesema kuwa vurugu hizo zilihusisha kundi la wanachama wa CHADEMA na wa CCM na zilisambaa ambapo wanachama hao walianza kurusha mawe ovyo na askari wachache wa polisi waliokuwepo, walizidiwa nguvu na makundi hayo.

Amesema katika kundi hilo ambalo wamelikamata,watawahoji na wataobainika kuhusika watafikishwa mahakamani wakati wowote.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

1 Comment

 

 

Add a comment

required

required

optional