UNAJUA KWAMBA MILLARD AYO ALIWAHI KUTOLEWA KATIKA CHUMBA CHA MTIHANI KWA KUTOMALIZIA ADA?
Kama tulivyokuahidi msomaji wa Mo blog ifuatayo ni sehemu ya pili ya mahojiano kati ya Mhariri wa Mo Blog Lemmy Hipolite na Mtangazaji maarufu Millard Ayo.
Mo Blog: Tunamsikia Millard Ayo lakini hatujui ni nani hasa.?
Millard Ayo: Milliard Ayo ni kijana wa miaka 26 aliyezaliwa tarehe 26 Januari mwaka 1986 ni kijana aliyezaliwa katika hospitali ya Mount Meru na ni mtoto wa kwanza kwenye familia ya watoto wanne.
Ninatoka katika familia ya Mzee Afrael Ayo al maarufu kama ‘Chalii’ pale Tengeru mkoani Arusha.
Mo Blog: Tupe siri ya mafanikio yako pamoja na umaarufu ulionao.?
Millard Ayo: Kiukweli moja kati ya vitu vinavyonifanya mimi nipate mafanikio, namshukuru Mungu kwa sababu kwanza situmii vitu vinavyowaangusha watu wengi kwenye kazi kama hizi; kwanza kabisa mimi sinywi pombe na sijawahi kunywa tangu nizaliwe; nadhani inanisaidia pia kwa sababu wakati wote akili inakuwa ‘fresh’.
Mo Blog: Kwa kifupi tuambie ilikuaje mara ya mwisho tumekusikia Radio One ghafla Clouds FM.?
Millard Ayo: Clouds Fm walivutiwa na kazi yangu, nadhani waliona uwezo wangu kupitia show ya ‘Milazo 101’ niliokuwa nikiifanya Radio One so alinipigia simu bosi wao nakumbuka ilikuwa ni siku ya Jumatano akaniambia tuonane.
Ukizingatia mimi nilikuwa na dream sana kufanya kazi ‘Clouds’ hata wakati naingia college ya Journalism nilikuwa na ndoto za kufanya kazi Clouds.
Mo Blog: Ayo tufafanulie kote ulikopita na hatimae hapa ulipo.?
Millard Ayo: Kiukweli nimefanya kazi TVZ Zanzibar, Wapo Radio -Dar es Salaam na ITV/Radio One kwa miaka mitatu; kote nilikuwa nafanyakazi na sisemi kwa nia mbaya, lakini Clouds ni Radio ambayo nilikuwa nimei’dream’ kuifanyika kazi kwenye maisha yangu.
Mo Blog: Zungumzia filamu za ki-bongo, kwa mtazamo wako tunaelekea wapi.?
Millard Ayo: Filamu za kitanzania zamani nilikuwa siangalii, lakini sasa hivi naangalia sana kwa sababu napenda kujifunza sana, mimi sikuzote napenda mtu ambaye anakubali kurekebishwa.
Filamu za kitanzania zina soko kubwa sana kwa watanzania, kwa sababu watanzania wanapenda vitu ambavyo wanavielewa; vitu ambavyo vina’happen’ kwenye maisha yao. Pia hakuna kitu kizuri kuwaona watu ambao unawafahamu wakiigiza inaleta uzalendo zaidi.
Mimi ningependa kuona waigizaji wa Tanzania wakitumia muda mwingi zaidi kujiandaa kwa ajili ya movie na waandaaji watumie fedha nyingi kutengeneza filamu ziwe na ubora unaostaili na naamini zitauza zaidi.
Mo Blog: Tupe siri ya sauti yako..?
Millard Ayo: Mwenyezi Mungu ndio anajua, Mwenyezi Mungu ndio muweza wa yote na Mwenyezi Mungu ndio aliyopanga kila ninachokifanya kwenye hii dunia. Amepanga niumbike au kuzaliwa niwe hivi. Najua kupitia Mwenyezi Mungu haya yote yamewezekana. Sauti yangu sijaitengeneza ni sauti ambayo nimezaliwa nayo.
Mo blog: Katika siku za hivi karibu kuna suala lililochukua nafasi kubwa katika midomo ya watu, suala la Freemason haswa kwa watu maarufu kama wewe. Unazungumziaje?
Millard Ayo: Mimi Freemason siijui naisikia tu kwa watu kwa hiyo siwezi nikatolea ufafanuzi zaidi kwa sababu sina elimu nayo, sijawi kushudia vitu kama hivyo kwa hiyo nawaachia wanaofahamu. Kwa kweli siwezi ku-comment’ chochote.
Mo blog: MO BLOG ingependa uzungumzie maisha yako ya kimapenzi maana tumesikia mengi.!
Millard Ayo: Wakati mwingine unapokuwa ni mtu wa kufahamika vinaweza vikazushwa vitu vingi sana, na kuna taarifa nyingi sana kuhusiana na maisha yangu ya kimapenzi ambazo sio za kweli.
Kiufupi ni kwamba mimi nina ‘girlfriend’ niko nae huu ni mwaka wa tatu sasa na ni huyo peke yake.
Mo Blog: Kumezuka utamaduni wa watu mbali mbali kufungua ‘Blogs’ hebu zizungumzie kama unavyozijua.
Millard Ayo: Kiukweli mimi napenda sana, kwanza watu wanaojituma kwa nguvu zao wenyewe . kufunguliwa kwa blogs nyingi kila siku sioni kama ni kitu kibaya ni kitu kizuri sana, kwa sababu kila mtu ana ubunifu wake, kila mtu ana nguvu yake. Cha msingi ni kufanya kitu ambacho kinaendana na lengo la kufunguliwa kwa blog. Napenda sana kuona blogs mbalimbali.
Mo Blog: Umekuwa mtangazaji muda mrefu sasa nini hutokisahau radioni?
Millard Ayo: Katika maisha yangu mimi sababu ya utangazaji nimewahi kufanya vitu vingi kwenye radio lakini kuna shows tatu ambazo siwezi kuzisahau ambazo niliweka nguvu nyingi sana. ‘Vipaji Halisi’-Wapo Radio, ‘Milazo 101’-Radio One na ‘Amplifaya’-Clouds FM.
Amplifaya ndio ninayofanya sasa hivi na nimeahidi moyoni nitazidi kuweka nguvu kuifanya vizuri zaidi kuanzia mwanzo hadi mwisho moto utakuwa uleule. Hii show sio kwamba naifanya kwa kuwa ni kazi hapana na-enjoy kufanya na nafurahi kuwa Clouds FM. Namuomba Mungu anipe nguvu.
Mo Blog: Changamoto gani unakutana nazo katika kazi wewe kama Millard Ayo..?
Millard Ayo: Kuna changamoto nyingi sana lakini labda kubwa ni pale ambapo ninataka niwe wa kwanza kutoa habari yaani nitoe ‘exclusive’. Hii ndio changamoto inayonifanya nichelewe kulala, ndio maana ukifungua web site yangu unaweza kuona nimeweka stori ya tukio lililotokea labda saa nane usiku. Ina maana nilikuwa eneo latukio. Napenda sana kuwa wa kwanza kutoa habari ‘always’.
Mo Blog: Kama Millard lipi tukio la kukumbuka sana duniani.?
Millard Ayo: Tukio la kukumbuka sana kwangu ni siku nipotolewa katika chumba cha mtihani wa kumaliza katika Chuo cha Uandishi wa Habari. Nilitolewa kwa sababu sikuwa nimemalizia kulipa. Baba yangu kipindi hicho gari yake ilikuwa imevamiwa na majambazi akipeleka watu mnadani. Lilipigwa risasi kwa hiyo likawa liko gereji. Ile hela ya akiba akawa ameitumia yote ikaisha na bado gari halikupona.
Halafu mama yangu ni mwalimu akawa amewalipia ada wadogo zangu waliokuwa wasoma katika hizi shule za Medium akawa hana pesa kabisa, yaani kwenda shuleni nilikuwa natembea wakati nauli ni shilingi 150/- au 200/-. Natoka Ngarenaro mpaka Stadium kila siku asubuhi na jioni kurudi nyumbani hata hela ya kula mchana inakosekana.
Baada kushindikana kabisa kupatikana ada, mama yangu akajaribu kwenda kuongea na wale masekretari ili wamkubalie nifanye mtihani kwa sababu alikuwa akijuana nao kinamna, lakini ikashindikana kwa sababu walikuwa wameachiwa maagizo kuwa siwezi kufanya mtihani mpaka nimalize ada na ilikuwa imebaki 300,000/-. Nikiamini mama atamaliza nao nikaingia katika chumba cha mtihani nikaanza kufanya baada ya kama dakika 10 au 12 hivi nikaja kutolewa tena nakumbuka ulikuwa ni mtihani wa ‘Video Shooting’.
Yaani nilipotolewa nikawa niko na mama analia mimi nalia nakumbuka nililia sana maana mtihani huo ulikuwa ndio-final, inamaana nisipofanya inabidi nisubiri tena mwakani. Mama akaniambia anakwenda asipopajua popote Mungu atakapo muongoza akatafute hiyo ada, basi nikamsubiri pale chuo chini kuna-kimgahawa nikalia sana mpaka dada mmoja aliyekuja kunihudumia chai akaniuliza unalia nini?
Akanibembeleza sana lakini nikawa nalia tu nashindwa hata kuongea akaniambia hata hiyo chai kunywa tu bure usilipe sema unataka nini kingine mi nikawa nalia tu.
Baada ya kama dakika 35 au 45 hivi nikamuona mama anakuja ‘speed’ anakimbia akitokwa machozi akaniambia nimepata hela mwanangu twende. Tukapanda tena mpaka ofisi ya chuo akalipa mimi nikaambiwa niende kwenye chumba cha mtihani.
Nashukuru kwamba somo lenyewe nilifaulu nilipata 93 kwa sababu nilikuwa nalipenda. Yaani jambo hili ndugu zangu wana Mo Blog sitakisahau.
Mo Blog : Pole sa ndugu yetu kwa kisa kilichowahi kukuta lakini ndio mitihani ya maisha.
Mo Blog: Millard unafikiria au kutamani kufanya kazi na radio gani nyingine..?
Millard Ayo: Kwa sasa sifikirii kwenda redio nyingine mimi bado niko Clouds na Clouds ni familia yangu.
Mo Blog: Tunakushukuru kwa muda wako kuzungumza na MO BLOG na tunakutakia mafanikio mema katika kazi na Mungu akubariki.
Millard Ayo: Akhsante sana wadau wangu.












at 11:40 am
millard MUNGU anampango na wewe..nimeumia sana kwa mkasa ulioupata. matatizo tumeumbiwa binadamu.
at 11:43 am
kwa kweli uwa napenda sana anavyospell jina lake bila kukosea, kijana mbunifu sana! nampa Saluti kama asemavyo mwenyewe, millard kaza buti bado kijana mdogo timiza ndoto zako.
at 12:01 pm
Tumeiona historia yako nadhani ni vizuri tukapata mafunzo toka historia za watu mbalimbali.Hongera sana
at 12:28 pm
safi sana millard, kwakuwa na ndoto nahati maye kuzitimiza
at 12:57 pm
I realy admire Milard Ayo he is very serious with his work and is very aggresive keep it up mdogo wangu, mtangulize mungu kwa kila jambo utafanikiwa hope you have many dreams don’t tired work work and work.
at 1:00 pm
Pole sana millard ayo kaza butu katika kazi achana na majungu nakipende san kipindi cha Amplify
at 1:31 pm
daaaah wa2 wanaptia meng sana ad wanafankiwa mh naamin hlo bt kaza buti bro sir GOD bbo anakupenda
at 1:35 pm
Pole xana kwa kutolewa ktk ama kwel kama ipo ipo tu… napenda xana unavyotangaza kaza but bro ayo….jamii hasa vijana wengi wana ndoto kama ulizo nazo je unatushaur vipi?
at 1:35 pm
POle sana Millard kwa yote uliyopitia binadamu siye
tumeumbiwa majaribu
at 1:37 pm
Nimejikuta natokwa machozi as if ndo umetolewa kwenye mtihani now
at 1:44 pm
pole sana. maisha ya binadamu Mungu pekee ndo anayajua……. usiache kumuomba sana mungu atakusaidia.
at 1:45 pm
daaaaa nimeipenda sana short history ya maisha yako…kila la kheri brodaaaaa
at 1:47 pm
Pole millard but yote ni life bro kaza kamba kiatu chako usilegeze
at 1:47 pm
inavutia kiukweli
at 1:57 pm
Pole sana kwa yaliyokukuta kijana kaza buti
at 1:58 pm
kza buti kijana mungu akubariki sna
at 2:00 pm
Ebwa ongera xana ongeza bidii iliuzidi kuwa mbunifu zaid
at 2:01 pm
Always i believe dreams will be true if someone put effort on it. Milard you are the great, keep it up! am on da way.from kaskazn.
at 2:07 pm
Dah pole sana Millard hiyo ni moja ya safari ya maisha cha kufanya usichoke kuendelea kumshukuru Mwenyenzi Mungu ndiye fanikio letu.
at 2:41 pm
Pole sn kwayaliyokukuta n Hongera sn kaka kwaulipofikia!…..Honestly natamani kuwa km wewe.
at 2:51 pm
jamani!nimeumia sana ulivyoongelea khs mama yako,mpende sana mama yako amejitahidi kutimiza ndoto zako,big up kwa kina mama wote!
at 3:05 pm
unajua ndoto njema huonekana asubuhi , hilo halina ubishi kamanda, cha kufanya muombe na kumshukuru aliyekuumba kwa kukubariki
at 3:09 pm
hakika kijana historia yako imenitoa machozi haswa pale ulipotolewa ktk chumba cha mtihani imeniuma sana kama mzazi ni kwa jinsi gani wazazi na familia inapata changamoto nyingi lakini sikuzote ikimtegemea Mungu hutaibika milele yeye ni mwingi wa huruma na yeye ndiye jibu ya matatizo yetu siku zote endelea kumtegemea yeye hakika utafika mbali sana
at 4:35 pm
Da,
kweli ukita mafanikio lazma upitie vkwazo kwanza
at 5:12 pm
Dogo kaza buti safari ndio kwanza inaanza!
at 5:36 pm
I do like Millard Ayo jaman! Mungu akupe maisha marefu
at 7:11 pm
Ebana kaka millad umegusa moyo sana kazabut sana brada
at 8:10 pm
i can’t really explain hw much i admire millard.. he z systematic, he z duing a really nice job… i wish every one in Tanzania 2b like Millard in duin any job.. becauz he z serius wth his work n he z working verry hard day 2 day.. feel so sorry 4wat happened 2u.. u were cryn but nw u’r smyln.. keep it up bro n stay blecd n live longer.
at 9:45 pm
Evry day u gv m a reasn z 2 y ur ma no 1 presenter.n dc intrvw a realse ur mo dan da best cz u hv bn thru a lot bt kpt n fightn n wd Godz help ur hu ur 2day n blv utafka mbl zaidi.blecd,talented,hardworkn,gud lokn,nyc voic…oooh millard wat else cn i say?hakunaga!!
at 11:34 pm
Evry day u gv m da reasn z 2 y ur ma best presenter n wd dc intervw a realise dat ur mo dan da best cz u hv had sm dficulties bt u neva gv up u fought n kpt on n wd Godz help ur hu ur 2day n stl blv utafka mbal zaid.talented,hardworkn,lovly voice,gud lukn…ooh Millard wat else cn i say?ur jst blecd, hakunaga!!!
at 4:45 am
Nimejikuta natokwa na machozi kwa kisa kilichokupata. Usimsahau mama maishani mwako. Mungu azidi kukutia nguvu Millard. Kaza buti you r still young
at 6:03 am
jamani nimeumia sana bt dats ril life en mpende sana mamako she deserve ur love Millard.
at 7:27 am
unamoyo wa kufanyakazi keep it up
at 10:10 pm
dogo uko juu tia nia na juhudi katika kazi na utafanikiwa zaidi big up dogo
at 5:38 am
Jamani usione vyaelea vimeundwa,Millard Mungu ni Mkuu sana jua hilo pale ambapo mwanadamu akili yake imefika ukomo ndipo Mungu hujitokeza,mama yako alikuwa na imani sana kwa Mungu,fata mfano wa mama yako utafanikiwa sanaaa! kumbuka wazazi wako utazidi kubarikiwa!
at 11:30 am
Jaman Millard…wish u lucky ma dr! Nakumbuka thoz days patandi yan umekua mkaka vibaya Mungu akutangulie ktk kila unalofanya!
at 3:12 pm
Thax
at 3:14 pm
Namkubali xna millard ayo kwa kaz nzur anayoifanya
at 3:42 pm
Hongera sana Millard. Changamoto katika maisha ni kawaida. Kwa nijuavyo, wengi wanaong’aa katika fani zao, historia zao za nyuma huwa ngumu sana. Mungu atakutangulia kaka.
Chukua changamoto zako kama sehemu ya kujifunza katika mambo yako mengine. Be blessed and congratulation once again.
at 6:47 pm
keep it up never give up kaka
at 6:53 pm
Katika yote hayo uliyoyapitia Ni Mungu peke yake ndio amekusaidia kukuvusha na kukufanikisha kuwa hapo ulipo kwa hiyo usimsahau Mungu hata kidogo katika maisha yako pamoja na kuwaheshimu wazazi wako kama biblia inavyosema waheshimu na baba na mama yako ili upate heri na siku nyingi dunian.Nakukubali sana kaka millard kwa kazi yako keep it up nevergive up.
at 6:54 pm
Katika hayo yote hayo uliyoyapitia Ni Mungu peke yake ndio amekusaidia kukuvusha na kukufanikisha kuwa hapo ulipo kwa hiyo usimsahau Mungu hata kidogo katika maisha yako pamoja na kuwaheshimu wazazi wako kama biblia inavyosema waheshimu na baba na mama yako ili upate heri na siku nyingi dunian.Nakukubali sana kaka millard kwa kazi yako keep it up nevergive up.
at 9:59 am
Mshukuru mungu kwa yote na pia mpende sana mama yako, na bila ya kumsahau pia baba yako na wote waliokufikisha hapo hulipo kwa sasa kaza buti mdogo wangu
at 4:47 am
dah pole sana ndugu ndo mithaniya Mwenyez MUngu hiyo ila naamini Mungu anakutangulia cn ktk maisha yk kwan kakuepusha na Mengi so uciache kumuomba kwa kila jambo ulifanyalo,kila la heri broo.
at 4:50 am
pole cn kaka ila naamini Mola yu pamoja nawe kila wakat, nakuombea heri tu ndugu yangu.
at 8:23 am
Nimefurahi sana kuifahamu historia ya maisha ya Millard Ayo,ofcourse me Millard ndio roll model na ningependa kuwa zaidi yake coz naamini nina kipaji cha utangazaji na nitasomea utangazaji kama millard!ningependa kuwasiliana zaidi na millard Ayo ili anipe ujuzi zaid!OFCOZ NAMKUBALI SANA BRO
at 8:26 am
Nimefurahi sana kuifahamu historia ya maisha ya Millard Ayo,ofcourse me Millard ndio roll model na ningependa kuwa zaidi yake coz naamini nina kipaji cha utangazaji na nitasomea utangazaji kama millard!ningependa kuwasiliana zaidi na millard Ayo ili anipe ujuzi zaid!
at 9:03 am
pole sana milard kwa hiyo short life history mimi kiukweli hata machozi yamenitoka kwa kusoma tu historia hiyo pole sana siku zote mwanzo mgumu laikini yote hayo yanashindikana na yanawezekana ila ukipambanana na kazi na kumtanguliza mungu mbele katika kila jambo lako hakuna kitakachoshindikana.muhimu sana ni mama kwa kweli hata siku moja mpambanie kwa kila jambo bila kumsahau mzee na ndugu zako.poaaaaaaaaaaaa.naitwa robert minja camera man itv kilimanjaro.
at 9:44 pm
wadau millard ni mtu wa nyota ya NDOO”aquarians” mafanikio yao hayaji kwa urahisi, ni wapambanaji wazuri sana na hawakati tamaa lakini ni wepesi sana kutokwa machozi. huwa hawatabiriki, wana sura nzuri za mvuto, wanapendwa na watu hasa akina dada kutokana na mvuto wa sura zao.keep it up bro.