THE CHOCOLATE CREW LAIBUKA MSHINDI SERENGETI DANSI LA FIESTA DAR,LAJINYAKULIA KITITA CHA SH MILIONI MOJA.

Kundi la The Chocolate Crew likishangilia kitita cha shilingi milioni moja mara baada ya kuibuka washindi kati ya makundi saba yaliyojitokeza kushiriki shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012,ndani ya kiota cha maraha cha Suncirro,Sinza jijini Dar.Katika shindano hilo kulikuwepo na ushindani mkubwa lakini mwisho wa siku mshindi ilikuwa ni lazima ajulikane/apatikane.Shindano hilo ambalo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya bia ya Serengiti ndio mdhamini mkuu wa tamasha kubwa lijalo la Fiesta linalorajiwa kuanza hapo baadae mara baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuisha.Shindano la namna hii limekwishafanyika katika mkoa wa Arusha ambapo mshindi lilikuwa kundi la Contegious Crew,mkoani Tanga kundi la Questions Crew waliibuka washindi pamoja na Viswani Zanzibar ambapo kundi la B-Six lilishinda.Aidha makundi yote hayo yalijinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.
Mmoja wa majaji na mratibu wa shindano hilo ajulikanae kwa jina la Msami akikabidhi kitita cha shilingi milioni moja kwa kundi la The Chocolate mara baada ya kuibuka kinara jioni ya leo kwenye ukumbi wa Sun Cirro,sinza jijini Dar.
 Baadhi ya mwashabiki wakishangilia
Mmoja wa watangazaji wa Clouds TV,Babu wa Kitaa kupitia kipindi Bibi Bomba akiwa amepozi na wadau wengine wa Clouds Media Group wakifuatilia shindano la Serengeti dance la Fiesta 2012.
Kundi la Mazabe Ndonga likionesha umahiri wa kucheza jukwaani kwenye shindano la kumsaka mshindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012,ndani ya kiota cha maraha cha Suncirro,Sinza jijini dar.Katika shindano hilo yamejitokeza makundi saba ambayo yameshindana vikali katika kumsaka kinara wao,zawadi katika shindano hilo ambalo mdhamini wake mkuu ni kampuni ya bia ya Serengi,ni fedha taslimu shilingi Milioni moja.Mashindano haya yamekwishafanyika katika mkoa wa Arusha ambapo mshindi lilikuwa kundi la Contegious Crew,Zanzibar likashinda kundi la B-Six na mkoani Tanga kundi la Questions Crew waliibuka washindi,aidha makundi yote hayo yalijinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.
Mmoja wa wasanii wa kundi la The Ridder akionesha mbwembwe zake kwa mashabiki kibao (hawapo pichani) waliofika kwenye shindano hili jioni ya leo,ambalo lilikuwa na msisimko mkubwa .
 Kundi la Tatanisha Dancers likisaka ushindi kwa udi na uvumba.
Baadhi ya washabiki waliojitokeza jioni ya leo kwenye shindano la kumsaka mshindi wa Serengeti dance la Fiesta 2012,ndani ya kiota cha maraha cha Suncirro,Sinza jijini dar
Mmoja wa majaji wa shindano hilo Isakwisha Thomson kutoka Clouds FM akifafanua jambo,kati ni Msami kutoka THT pamoja na B-Dozen kutoka Clouds FM,Wote ndio waratibu wa shindano hilo la Serengeti dance la  Fiesta 2012.
Kundi la Manzese Crew  likisaka ushindi kwa udi na uvumba jukwaani kuwania kitita sh milioni moja. 
 Mashabiki wakifuatilia shindani hilo jioni ya leo.
 Kundi la Chocolate lionesha mbwembwe zake jukwaani kuwani kitita cha shilingi milioni moja.
 Mmoja wa majaji katika mashindano hayo Isakwisa Thomson akielezea jambo wakati shindano likiendelea.
 Mc wa shindano zima,Nickson akiwayataja makundi yaliyotinga fainali kwenye mchakato wa kulipata kundi kinara la Serengeti dance la Fiesta 2012.
 Majaji wakijadiliana jambo kumpata mshindi
Palikuwa hapatoshi jioni ya  leo ndani ya ukumbi wa maraha wa Sun Cirro,Sinza jijini Dar.
 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional