Bango la mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.Picha na Nathaniel Limu.
Na Nathaniel Limu.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Miyombwe kijiji cha Mkinya jimbo la Singida Mashariki Michael Andrew Khaliki (53), amehukumiwa adhabu ya kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa shilingi laki moja, iliyokuwa itumike kugharamia ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Dung’unyi.
Mapema mwansheria wa TAKUKURU mkoa wa Singida Antidius Rutayuga alidai mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Tyephosofia Tesha kuwa mnamo septemba 16 mwaka 2008 huko katika kijiji cha Mkinya, mshitakiwa alipokea shilingi 180,000 kutoka kwa Elias Kiemi ikiwa ni mchango wa familia yake kwa ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Dung’unyi,
Amesema kati ya fedha hizo mshitakiwa Michael alitumia shilingi laki moja kwa matumizi yake binafsi jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Mwanasheria huyo wa TAKUKURU alisema kuwa hata hivyo, mlalamikaji Eliasi alifanya juhudi kubwa kudai stakabadhi ya mchango wa shilingi laki moja kutoka kwa mshitakiwa Michael, lakini hata hivyo, juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda na kupelekea afike ofisi ya TAKUKURU mkoa,kutoa taarifa.









at 8:24 am
liwefundishwe kwa mafisdi wengine…
at 8:37 am
ona sasa sheria za Tanzania zinavyopendelea!huyu mzee maskini kaiba lak 2 kapigwa jela miaka 2,na jana wale wezi wakubwa mafisadi walioiba zaidi ya bilioni 2,wamefungwa miaka 3,hv kuna uwiano hapa?
at 8:59 am
ona sasa sheria zetu zinavyopendelea huyu kaiba laki 2 kahukumiwa 2yrs,wakati wale mafisadi walioiba zaid ya 2 bilion wamehukumiwa 3yrs only,hivi kuna haki hapa?