BENKI YA NMB KUTOA MAFUNZO YA UELEWA WA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI MKOANI SINGIDA.

Meneja biashara wa benki ya NMB tawi la Singida Noel Malya akitoa mada yake ya kuhamasisha wanafunzi kuanza kujijengea utamaduni wa kuweka akiba benki.

Afisa huduma kwa wateja wa benki ya NMB tawi la Singida Rose Makukuru akitoa mada yake ya kujifunza kuweka fedha benki katika umri mdogo kwa wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Unyankindi na Singidani mjini.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Singidani na Unyankindi waliohudhuria uzinduzi wa mpango wa NMB Financial Fitness’ uliofanyika kwenye shule ya msingi ya Unyankindi. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Benki ya NMB tawi la Singida imezindua mpango wa ‘NMB Financial Fitiness’ ambao pamoja na mambo mengine, unatoa mafunzo ya uelewa mpana wa matumizi sahihi ya fedha kwa wanafunzi wa shule za msingi mkoani Singida.

Meneja wa tawi la NMB Singida Christina Mwangomo amesema madhumuni ya benki hiyo kuanzisha utoaji wa mafunzo hayo ni kuwajengea  wanafunzi wa shule ya msingi uelewa wa matumizi sahihi, na kuwajengea mapema mazingira mazuri,  ili waweze kutumia fedha kwa uangalifu.

Katika hatua nyingine Meneja huyo amesema NMB ina mpango wa kuwajengea wateja wake na jamii, msingi ambao utawezesha kuwa na uelewa, umakini wenye uhuru wa kuchagua jinsi ya kuhifadhi fedha, kuwekeza au kukopa na kufanya maamuzi sahihi ya kuchagua benki inayofaa.

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo Meneja biashara wa NBM Singida Neol Mlay ametaja baadhi ya mada zitkazotolewa kuwa ni pamoja na NMB Financial Fitness ni nini, Je kwa nini watu wanaweka fedha benki, kesho inaanza leo ina maanisha nini na akaunti ya watoto iliyopo NMB.

Kwa upande wake Afisa huduma kwa wateja wa tawi hilo Rose Makukuru, amesema kupitia mpango huo, wanatarajia wanafunzi watajifunza kuweka akiba katika umri mdogo.

Kwa mujibu wa Rose, NMB kupitia sera yake ya msaada kwa jamii, ipo kwa ajili ya mambo makubwa matatu ambayo ni Elimu, Afya na Michezo. 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional