Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Myway Entertainmet iliyoandaa tamasha hilo Paul Mganga (kulia) akizungumzia lengo ni kudumisha utamaduni wa mtanzania kwa kuwaleta watu wa makabila mbalimbali na kuwakumbusha utamaduni wao, kujenga na kudumisha mahusiano baina ya makabila mbalimbali nchini tanzania na pia kutangaza na kuimarisha misingi na maadili ya makabila ya kitanzania.
Akifafanua zaidi Mganga amesema wanaimani kuwa zaidi ya watu 3,000 na familia zao watahudhuria kwa wingi tamasha hilo la kihistoria ambapo watapata fursa ya kusikia historia ya wachagga kwa kina kutoka kwa wazee wa kichagga watakaokuja kutoka mkoa wa Kilimanjaro.
Amesema pia wataona na kucheza ngoma zote za asili za kichagga na kula aina zote za vyakula vya asili vya kichagga.
huku vyakula na vinywaji vya asili kutoka mkoa wa Kilimanjaro, Kiburu, ndafu, shiro, kitawa, macharari, ngararimo, ng’ande, kisusio, mtori, Kisusio na vingine vingi vitakuwepo siku hiyo.









at 6:22 am
shuld do it again and advertise it in the medias many of us didnt knw!!
at 5:34 pm
nimeipenda hiyo siku ya wachaga ila tuwe tunaambiana.its me lyatuustan from ttc kantalamba