SERIKALI ISIPOJIGUSA..!! MGOMO WA WALIMU KUANZA JUMATATU TAREHE 30 JULAI 2012.

 

Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwl. Gratian Mukoba akisisistiza kuwa mgomo wa waalimu ni halali hauna uhusiano na zoezi la Sensa . Kulia ni Makamu wa rais wa Chama hicho Mwl. Honoratha Chitanda.

Baadhi ya walimu wakisimsikiliza rais wa CWT.

Na.MO BLOG TEAM

Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kimesema kwa kuzingatia Kifungu cha 80-(1) (d) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Mwaka 2004, walimu wanachama wa CWT walianza zoezi la kupiga kura tarehe 25 Julai 2012 kama ilivyoelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa baada ya kura zote kupigwa , asilimia 95.7 ya wanachama wameunga mkono mgomo, ambao ni walimu wanao fundisha katika shule za awali, msingi, sekondari, maafisa walioko kwenye ukaguzi wa shule za awali, msingi, sekondari, maafisa walioko kwenye ukaguzi wa shule na wakufunzi wa vyuo vya ualimu na maendeleo ya jamii.

CWT kimetoa wito kwa walimu wote kuunganisha nguvu kudai haki yao stahili bila kujali vitisho vinavyoendelea kutolewa.

 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

14 Comments

  • Safari hii, MIMI NIKO TAYARI KWA CHOCHOTE. Kama ni kunifukuza, nyie nifukuzeni tu. SIENDI KAZINI NG’O.

     
  • Mwl philemon Sokime

    Mgomo wa walimu ni sahihi kabisa.Cha msingi maafisa elimu mnaozuia mgomo acheni huo unafiki wenu,nyie sio serikali, ni vibaraka tu.Tukifanikiwa kupata maslahi yetu,je, nyie maafisa mtakataa hayo maslahi? Acheni unafiki wenu! nyie si waajiri wetu. Walimu tuungane turudishe heshima ya fani ya ualimu

     
  • TICHA omy

    mgomo kama kamakawa
    SERIKALI KWANINI HAMTAKI KUTU SIKILIZA

     
  • Mwl G.K

    Wazazi na wanafunzi tunaomba msitufikirie vibaya,tunachodai serikalini kitatufanya tufanye kazi kwa ufanisi ili nanyi mpate manufaa.

     
  • mwl Hamisi

    mgomo umechelewa sisi mwanza tuligoma zamani hata rais usingetangaza mgomo ulianza mapema na tunasubiri kwenye mitihani yao ya sekondari mm na digree yangu unanipa laki 3 tena walimu umoja ni nguvu utengano udhaifu

     
  • STAIMILI OMARI KIPOZI

    KWAKUWA TUNATIMIZA WAJIBU , NA HAKI YETU TUPEWE.

     
  • Mambo vipi wazee wazee wa forum?

     
  • Sell ngassa D

    Mgomo ndo suluhisho coz if diplomacy fails coersive can quickly do, but nna wasiwai na walimu mana most of them are coward tena nasikia kuna baadhi ya mazuzu yameenda kazini. inabidi wachunguzwe huenda vyeti vyao ni vya kuchakachua.ndg walimu there’s no success without sacrifice

     
  • mwalimu ntuzu

    Walimu kama kawa.

     
  • Innocent Reuben Baligono.

    Ukweli ni kwamba walimu tumechoka na hatuko tayari kufanya kazi katika manzingira haya ya kulipwa mishahara kidogo, serikali inabidi ijifunze kupitia huu mgomo na si kutoa vitisho kwa walimu wakati ukweli wanaujua!

     
  • Ediga

    MGOMO NI HATUA YA MWISHO KATOKA MAKUBALIANO, HIVYO SERIKALI IONE KUWA WATU WAMECHOKA. NINGEWASHAURI WAFUNGUE POCHI WATOE HIZO FEDHA.

    WALIMU ARUTA CONTINUE. MGOMO MPAKA KIELEWEKE

     
  • Anonymous

    walimu waengezewe mshahara, wapewa makazi safi ya kuishi huduma za jamii ziwepo, mbona mnaduwa nyie wana wa si-hasa bila walimu hata hizo siasa msingeziweza.mnatulipa mshaara wa robo ya madaktari. mnyonge mnyongeni hakiyake mpeni.

     
 

 

Add a comment

required

required

optional