Rais Kikwete akishiriki katika swala ya kumuombea marehemu mjini Lindi leo Julai 30, 2012.
Aidha, rais Kikwete amehudhuria mazishi ya shemeji yake , Marehemu Amani Kinyozi, aliyefariki siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete, ambaye ameongozana na mke wake Mama Salma Kikwete, alijumuika na mamia ya wakazi wa mji wa Lindi kwenye mazishi hayo, yaliyofanyika katika makaburi ya Mitandi, mjini humo.
Marehemu Amani Kinyozi, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 45, ameacha mke na watoto wawili.
Enzi za uhai wake marehemu alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mifuko ya karatasi, na pia alikuwa akifundisha kinamama wajasiriamali ufundi huo katika juhudi za kuepukana na matumizi ya mifuko ya plastiki, maarufu kama mifuko ya rambo ya kufungia bidhaa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
30 Julai, 2012









