Baloteli akiwasili uwanjani hapo kabla ya kuzongwa na mashabiki lukuki.
Mario ilibidi aokolewe na wafanyakazi wa uwanja huo kama hapa anavyoonekana akiambiwa sasa shwari waweza kutoka.
Mmoja wa wafanyakazi wa Uwanja huo akimsaidia kuburuza begi lake na kumuonyesha njia salama ya kutokea kuelekea gari lilikokuwa likimsubiri.
Mario akitabasamu wakati akiagana na wafanyakazi wa uwanja wa ndege ambao walitumia uwezo wa hali juu kumuokoa.
Mchezaji mahiri ya klabu ya Manchesta City ya Uingereza Mario Baloteli alilazimika kutafuta hifadhi ya muda katika moja vyoo vya uwanja wa ndege wa Manchester akiukimbia umati wa mashiki alioogopa kuwa watamzonga.
Baloteli mwenye umri wa miaka 21 anayefahamika kutoa maneno ya hovyo awapo uwanjani alikuwa akiwasili uwanjani hapo akitoa Milan nchini Italia.
Mchezaji huyo mtata alikuwa amesimama na rafiki yake sehemu ya wageni wanaowasili akisubiri begi lake akijua hakuna mtu atamshitukia.
Bahati mbaya alionekana na mashabiki wa Machester City ambao alimzonga wakitaka kupiga picha na kuwekewa saini yake katika vijitabu vyao.
Baada ya umati kuwa mkubwa mchezaji huyo alishindwa kuwahimili na ikabidi atumie njia mbadala ya kutoka nduki na kujifungia moja ya vyoo vya uwanja huo.












at 11:14 am
Huyu kijana umaarufu wake unatokana na vioja, he rarely make headlines of football nature.