MRATIBU WA SENSA WILAYA YA SINGIDA AHIMIZA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO WAKATI WA SENSA.

Mratibu wa sensa wilaya ya Singida,Nevilling Lyimo,akihamasisha zoezi la sensa taifa katika kijiji cha Ikungi jimbo la Singida mashariki,inayotarajiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Mratibu wa sensa wilaya ya Singida Nevilling Lyimo amewahimiza wananchi kuhakikisha watu wote wenye ulemavu mbali mbali wanahesabiwa bila kukosa Agosti 26 mwaka huu.

Lyimo ametoa changamoto hiyo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu sensa ya kitaifa inayotarajiwa kufanyika Agosti 26 mwaka huu.

Amesema walemavu wa aina yeyote, wana mahitaji ikiwemo kuendelezwa sawa na watu wasiokuwa na ulemavu wo wote, hivyo kuhesabiwa ni jambo la lazima kwao.

Katika hatua nyingine, Lyimo amesema katika kuhakikisha kuwa kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu, kuna makundi mbali mbali ya watu ambayo yanatakiwa kuhamasishwa ili yatoe ushirikiano mzuri katika kufanikisha kazi ya kuhesabu makundi hayo.

Ameyataja makundi hayo kuwa ni wawindaji, wavuvi, wachungaji wanaohama hama, watafutaji madini na baadhi ya wakulima ambao wana mashamba yaliyo mbali na makazi yao ya kawaida.

Aidha, Lyimo amesema watu watakaosafiri siku ya kuamikia siku ya sensa, wao watahesabiwa pale watakapoanza safari au watakapomalizia safari zao.

Kauli mbiu ya sensa ya mwaka huu, ni ‘Sensa kwa maendeleo, jiandae kuhesbiwa.

 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional