MWOGELEAJI WA CHINA ALIYEVUNJA REKODI OLIMPIKI AKANA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU.

Mwogeleaji kutoka China mwenye umri wa miaka 16 Ye Shiwen amekanusha kutumia dawa za kuongeza nguvu baada ya kuvunja rekodi ya dunia katika michezo ya Olimpiki inayoendelea jijini London.

Ye ameshinda Medali ya Dhahabu ya kuogelea mita 400 ambapo alivunja rekodi yake mwenyewe kwa takriban sekunde tano.

Hata hivyo hakuna ushahidi dhidi yake na washindi wote wa medali wamepimwa.

Ye Shiwen leo anatarajiwa kushindana katika fainali za kuogelea mita 200.

 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional