WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA CHACHU YA KUFANIKISHA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akifungua mafunzo ya siku mbili yaliyohusu sensa ya taifa kwa waandishi wa habari 163 (hawapo kwenye picha) wa kanda ya ziwa na kanda ya kati.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya sensa taifa mkoani Mwanza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza (aliyeketi katikati) Injinia Evarist Ndaikilo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Singida.

Jengo la hoteli ya Annox ya jijini Mwanza mahali wafunzo ya sensa kwa waandi wa habari yalifanykia.

Sehemu ya jiji la Mwanza. (Picha zote na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu.

Waandishi wa habari nchini wamehimizwa kuongeza kasi katika kutumia kikamilifu kalamu zao kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki zoezi la sensa ya mwaka huu, ili lengo liweze kufikiwa.

Changamoto hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo, wakati akifungua mafunzo ya sensa ya watu na makazi kwa waandishi 163 kutoka mikoa minane ya kanda ya ziwa na kati.

Amesema serikali inatambua wazi mchango mkubwa unaotolewa na waandishi wa habari wa kuhamasisha maendeleo ya wananchi pamoja na kuwaelimisha umuhimu wa kushiriki matukio mbali mbali ya kitaifa ikiwemo la sensa.

Amesema kwa hali hiyo, waandishi wa habari wana wajibu wa kuwaelimisha wananchi waelewe kwa kina, kuwa sensa ya watu na makazi, ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote waliopo nchini ambapo taarifa zao za kijamii na kiuchumi, hukusanywa. 

Sensa pia hukusanya hali ya makazi ya watu hao.

Mkuu huyo wa mkoa amesema iwapo waandishi wa habari watatimiza wajibu wao huo, watakuwa wameisadidia serikali kuweza kufahamu mahitjai ya wananchi wa kila rika na mahali walipo.

Awali, Mratibu wa mafunzo hayo kutoka ofisi ya taifa ya takwimu makao makuu Said Ameir, alisema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo zaidi wa kufahamu kwa kina malengo/madhumuni ya zoezi la sensa ya taifa inayotarajiwa kufanyika agosti 26 mwaka huu.

Alitaja baadhi ya mada zitakazotolewa kuwa ni pamoja na umuhimu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 na maandalizi yake, maeneo ya kuhesabu watu, sheria ya takwimu na wajibu na majukumu ya vyombo vya habari katika kufanikisha zoezi la sensa.

 Mafunzo hayo yaliandaliwa na kufadhiliwa na ofisi ya taifa ya takwimu, yamefanyika kwenye ukumbi wa mkutano wa hoteli ya Annox, jijini Mwanza.

 

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional