Mkazi wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa kijiji hicho kilichopo wilayani Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo, katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam. Kushoto anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.
Mama Maria akimkabidhia funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi kwa mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha, diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma, Alhaj Omar Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa trekta kumi kwa wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam.
Diwani Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
Pokea japo kidogo, mkoba huu ni wako Mama Mpendwa.












