DR. KONE ATOA WITO KWA WATALAAM KUANZA KUWAANDA WATANZANIA KUWA NA MAKAZI YA MAGHOROFA ILI KULINDA MAENEO YA KILIMO.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua  maoni kutoka kwa   Mhasibu wa Wizara ya Fedha Abbas Myeto(kulia) kuhusu taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wa umma wanapostaafu . Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida aliomba ufafanuzi huo leo  alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitaka kujua mjini Dodoma kutoka kwa watendaji wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) kwanini kuna utofauti wa ubora katika bendera ya Taifa ya kuweka katika magari kwa viongozi. Mkuu Mkoa huyo aliuliza swali hilo jana  alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma. Aliyeshika bendera ndogo ya taifa ni Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia).

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akipata maelezo mafupi  jinsi  Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini [GPSA] inavyosaidia katika kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyokuwa yakifanyika kupitia ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya ofisi za serikali na taasisi zake. Mkuu Mkoa huyo alipata maelezo hayo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Menejimenti ya Mikataba Maalum Modecai Mato (kulia) alipotembelea banda la Wizara ya fedha katika maonyesho ya wakulima kitaifa ya nanenane yanayoendelea mjini Dodoma.

Mchambuzi wa Mifumo ya Komputya Mkuu Daraja la III kutoka Idara ya Menejimenti ya TEKNOHAMA ya kifedha , Wizara ya Fedha Margethi Ambrosi Nembo (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dr.  Parseko Kone (kulia) mjini Dodoma jinsi kuingiza mishahara na malimbikizo ya watumishi wa umma kwa kutumia TEKNOHAMA . Mkuu Mkoa huyo alikuwa katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Meneja Mawasiliano na Kumbukumbu wa Shirika Hodhi la Mali ya Mashirika ya Umma (CHC)  Joseph Mapunda (kushoto) akimpa  Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kulia) jinsi Shirika hilo linavyofanya tathmini ya mashirika ya umma yaliyobinafsishwa na utendaji wa mashirika hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Afisa uhusiano na Masoko wa Chuo cha Mipango Dodoma Godrick Ngoli (kulia) akimpa  Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kulia) jinsi Chuo hicho kinavyotarajia kutoa kozi mbalimbali zinahusu mazingira ili kukabiliana na changanoto ya ongezeko la watu haoa nchini . Mkuu huyo wa Mkoa alipata maelezo hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dr.  Parseko Kone (kushoto) akitoa changamoto kwa watumishi wa Chuo cha Mipango cha Dodoma kuwa na mitaala ambayo itawaandaa wananchi kuanzia ngazi ya chini juu ya kuwa na mipango mizuri ya matumzi bora ya ardhi ili kukabiliana na ongezeko la watu nchini. Mkuu Mkoa huyo alitoa kauli hiyo mjini Dodoma alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya wakulima nanenane mjini Dodoma.(Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma).

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone ametoa wito kwa Taasisi za elimu nchini kuandaa wataalam watakaobuni mipango ya ujenzi wa nyumba ambazo zinachukua eneo dogo lakini zinauwezo kuchukua idadi kubwa ya watu( Ghorofa).

Hatua hiyo itasaidia wananchi mbalimbali kutojenga katika maeneo ambayo ni muhimu katika uzalishaji wa mazao mbalimbali .

Mkuu wa Mkoa huyo alitoa kauli hiyo leo mjini Dodoma alipotembelea Chuo cha Mipango cha Dodoma katika banda Wiazara ya Fedha katika maonyesho ya nanenane .

Alisema kuwa Taasisi za elimu zitakiwa kuzalisha watalaam watakaosaidia wananchi kujenga nyumba ambazo zinachukua eneo dogo na zinaendea juu au chini ili kufanya maeneo ya kilimo yaendelee kuwa shughuli ya uzalishaji wa mazao .

Dr. Kone alisema kuwa utaratibu wa hivi sasa wa kila mtu kuchukua eneo kubwa na kujenga nyumba ambayo inachukua idadi ndogo ya watu unasababisha watu wajenge hata katika maeneo muhimu ya uzalishaji wa chakula ambayo ni hatari kwa maisha ya baadae ya watu katika suala la upatikanaji wa chakula na mazao mengine.

Alisema kuwa miaka 15 ijayo kama jitihada zisipochukuliwa uwenda sehemu kubwa ya maeneo ya kilimo ikajaa majengo kutokana na ujenzi wa nyumba zinasambaa kila sehemu  na kufanya eneo la uzalishaji wa mazao kuwa dogo kuliko la makazi .

Dr. Kone aliongeza kuwa ni vema eneo ambalo linastahili kwa uzalishaji wa mazao mbalimbali libaki na shughuli ya kilimo badala ya kukimbilia kulijenga na ujenzi ufanyike katika maeneo ambayo hayafai katika shughuli za kilimo.

Hivyo ameomba watalaam kutokuwa waoga katika kuangaa mipango ambayo faida zake zinataa kuonekana miaka mia moja(100) ijayo.

Mkuu wa Mkoa huyo alisema kuwa hivi sasa ni vema watalaan wakaangalia utaratibu mpya wa mazishi ili ikiwezekana badala makaburi kuwa na eneo kubwa basi kuwepo na utaratibu wa kuchoma moto.

Maonyesho ya wakulima ya nanenane yanatarajia kufikia kilele siku ya Jumatano 8.8.2012 ambapo Kitaifa yanafanyika mjini Dodoma.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional