Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra Agosti 11, 2012 baada ya kumtembelea na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills aliyezikwa Ijumaa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais John Dramani Mahama wa Ghana nyumbani kwake jijini Accra Agosti 11, 2012 wakati alipomtembelea kiongozi huyo mpya wa Ghana na kumpa pole ya msiba wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Marehemu John Evans Atta Mills.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama manasi yakitayarishwa kwa ajili ya kusafirishwa na kuuzwa nje ya nchi katika kiwanda cha Bomarts Farms Ltd. katika kitongoji cha Dobro nje kidogo ya jiji la Accra Agosti 11, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitazama ukulima wa kisasa wa manasi yanayolimwa kwa ajili ya kuuzwa nje ya nchi katika shmaba la Bomarts Farms Ltd. katika kijiji cha Dobrokatika eneo la Nsawam nje kidogo ya jiji la Accra Agosti 11, 2012. Kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa shamba hilo Bw. Anthony Botchway na mwenye suti ya buluu ni Waziri wa Chakula na Kilimo Mhe Kwesi Ahwol.












