Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo, George Nyatogo.
Na Joachim Mushi, Thehabari.com
BODI ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imewaengua zaidi ya wanafunzi 3074 walioomba vyuo na mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2012/13.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na taasisi hizo kupitia mitandao yao (website) Agosti 10 na 12, 2012 zaidi ya wanafunzi 3074 wameenguliwa katika maombi yao kwa kuwa na dosari mbalimbali.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) pekee imeorodhesha zaidi ya wanafunzi 2,649 ambao imebaini kuwa na mapungufu kadhaa katika maombi yao ya kupewa mikopo ya vyuo.
Miongoni mwa makosa ama dosari ambazo bodi imezibaini kwa walioenguliwa kwa sasa ni pamoja kukosekana kwa vyeti vya kuzaliwa kwa muombaji, sahihi ya mdhamini/muombaji, kukosekana kwa picha ndogo ya muombaji/mdhamini, kukosekana kwa sahihi za viongozi wa Serikali za mitaa/vijiji kwa waombaji na nyaraka nyingine muhimu kwa waombaji.
Kwa upande wake TCU imewaengua jumla ya waombaji 425 kwa dosari na makosa mbalimbali, ambayo imeyabainisha katika taarifa yake.
Miongoni mwa dosari ambazo zimetajwa na TCU kwa wanafunzi hao ni pamoja na baadhi yao kukosea namba za vyeti vya masomo kwa vidato vya nne na tano (O’ level na A’ level Index number), miaka ya kumaliza masomo (year of completion), mawasiliano sahihi kwa muombaji (Contact information e.g. Mobile phone number, email address and postal address) pamoja na uchaguzi wa masomo (Programme selected).
Waweza kuingia katika linki hii hapo chini na kuona majina ya waliobainika kuwa na dosari anuai katika maombi yao kwa TCUhttp://www.tcu.go.tz/uploads/
Pia waweza kutembelea linki zifuatazo na kushuhudia majina ya waliobainika kuwa na dosari hizo katika maombi yao kwa bodi ya mikopo;-http://www.heslb.go.tz/index.
post graduate;- http://www.heslb.go.tz/index.
Hata hivyo taasisi hizo mbili zimetoa muda kwa walioenguliwa sasa kutokana na dosari hizo kurekebisha na kutuma tena maombi yao kupitia mitandao kwa mujibu wa maelekezo waliyotoa. Kwa taarifa zaidi pia waweza kutembelea mitandao ya www.heslb.go.tz na www.tcu.go.tz
Habari hii imeandaliwa na mtandao wa Thehabari.com (www.thehabari.com)









at 8:50 pm
Tusaidieni jamani watu tuliokosa mkopo mwaka jana tupate mkopo nimemaliza mwaka wa kwanza kwa kukopakopa hela nilipe ada hata sijui mwaka huu nitalipa nini nawaombeni mkopo lydia mbilinyi tumain university makumira arusha
at 8:16 am
bodi ya mikopo mmefanya uamuzi mzuri wa kutoa list ya waliokosea kwenye kufanya application zao coz without doing that many student wangekosa mikopo,bigup
at 3:28 pm
kwakweli nyie mnaubaguzi kwan mkitoa hiyo mikopo bila ubaguz mtapungukiwa na nn? wakati wakwenu mmewapatia bila makwazo yeyote
at 9:19 am
i want to know if there is miserrors in my loans application forms
at 3:13 am
I think the Board has done a great thing!!
at 5:23 am
loan board big up, coz mmefanya kitu cha huruma kutoa majina ya waliosahau baadhi ya viambatanisho,na sahihi, maana huu ni uzembe wao, mngeweza kuwapiga chini,
at 6:50 pm
loan board big up, coz mmefanya kitu cha huruma kutoa majina ya waliosahau baadhi ya viambatanisho,na sahihi, maana huu ni uzembe wao, mngeweza kuwapiga chini,
at 7:09 am
jaman Bodi naomben kujua kama nimepata mkopo,kwani mambo ni magumu sana kitaaa….na kwaatakae ona chochote anambie kuhusu mimi.
at 8:52 am
kwa nini msitoe na majina ya waliofanikiwa na kiasi walichopata mapema ili watu waweze kujiandaaa mapema? Acheni ubabaishaji kujifanya Mungu watu……..
at 5:34 pm
sana tu wachane hao washatuona sisi tunajibembeleza sana mafisadi wakubwa hao
at 9:00 am
dah hivi upo uwezekano kweli wa kupata mkopo hapo maana 3000 sio mchezo
at 2:38 pm
gud thing mmetoa majina ya waliokosea but mnge consider course zote kwenye utoaji wa mkopo sababu mtu anaweza faulu ila kisa anataka kuwa journalist au course nyingine hawezi pewa mkopo uwo ni uwonevu naomba mjipange upya na condition zenu
at 2:41 pm
mgawe mkopo kiusawa na course nyingine wanufaike sio mnawapa walimu ,doctor na engineer tu siyo fair kwani wengine hatuna shida?
at 6:03 pm
mbona mnachelewesha mambo watu tujue mwelekeo
at 11:43 pm
Hongera kwa bodi ya mikopo kutoa muda wa marekebisho ila tunaomba mutuongezee muda kwani muda mlio utoa hautshi
at 11:41 am
Hongereni sana kwa kazi ya kubaini waliokosea na kuwapa muda zaidi wa kufanya marekebisho,mimi binafsi naomba mtoe mkopo kwa waombaji wote walioomba mkopo kwa usahihi kwa sababu wengine wanatoka katka familia za hali ya chini sana kiasi kwamba hazina uwezo kabisa wa kumudu gharama za chuo mfano mzuri ni mimi mwenyewe nlimaliza mwaka jana nikachaguliwa IFM lakini kutokana na uwezo mdogo wa kifedha sikuweza kuripoti chuoni nikaamua kuahirisha hadi mwaka huu kwahiyo basi napenda kusisitiza kutoa mkopo kwa wanafunzi ambao hawakuweza kuripoti katka vyuo walivyo chaguliwa miaka iliyopita kwa sababu hiyo ni ishara tosha kuwa hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama za chuon na ninafahamu mikopo ni kwaajili ya wanafunzi wasio na uwezo,naimani ombi langu litapewa kipaumbele,kila la kheri katka ujenzi wa Taifa
at 9:18 pm
Mmefanya jambo la maana,bg up!ila ningeomba walioshndwa kuripot kurport kwenye vyuo mwaka jana kwa sabab za kfedha’mi mmojawapo’ tupewe kpaumbele.
at 6:43 am
kila mtu yuko sawa bwana si zani kama tunazidiana uwezo kwa hiyo wote tupewe mkopo sawa kwa sawa jamani, mtatuumiza.
at 7:28 am
why wamechelewesha kutoa majina haya. sio poa wanavyofanya na wakati asilamia 90 ya waombaji ni masikini. watasomaje jamani
at 10:47 am
Big up loan body you have done a great thing!!!
at 2:12 pm
JAMANI WOTE 2PEWE MKOPO KWANI WOTE 2NASHIDA SANA . MAISHA MAGUMU KWA WOTE.NA KAMA WOTE TUKIWA WALIMU ,MADAKTARI JE WANASHERIA WTATOKA WAPI? NA FANI ZINGINE ZITAONGOZWA NA NANI?
at 6:51 pm
kwa nini msitoe na majina ya waliofanikiwa na kiasi walichopata mapema ili watu waweze kujiandaaa mapema? Acheni ubabaishaji kujifanya Mungu watu……..
at 5:15 am
makosa mengine niyakujitakia,unaomba mkopo wakati ww mwenyewe unasahau kuweka sahihi yako,kiboksi cha picha kipo na bado hujaweka,serekali za mitaa hujapeleka,
“JAMANI HATA KAMA AKILI HUNA MACHO HAYAONI”
ww ni msomi wa aina gani? na ulivukaje ulipotoka?
at 8:46 am
ucseme hvyo kusahau kaumbiwa binadamu hizo zako ni dharau
at 6:41 am
taarifa zenu nzuri tutawajulisha na wengine
at 8:38 am
mnyonge mnyogeni haki yake mpeni! ni lazima tuelewe watanzania wengi income yetu ni ndogo sana, so kwa tuliotoka katika familia za kimaskini,tunaomba mtufikirie sana LOAN BOARD.Bila ivyo tutashindwa ku survive
at 9:22 am
NO COMMENTS
at 5:50 pm
JAMAN IV KAWAMBWA HAKUMBUKI 2LIPOMKALISHA JUAN MWAKA JANA UDSM? PALE MLIMN. POA 2 ILA KYAMA KYAJA 2TAFANIKIWA TU POLEN WADOGO ZANGU…….
at 7:54 am
muache ursimu tendeni kazi yenu kwa uwadilifu
at 8:50 am
ww haujui ulisemalo kwani kusahau waliumbiwa fisi hizo ni dharau
at 9:59 pm
MWAKA HUU MMETUWEZA HV MIKOPO INATOREWA KWA WATU AINA NGAN KWAN MWAKA JANA NIMEKOSA MWAKA HUU NAPENYEWE JAMANI NIONEINI HURUMA NA MIMI MTOTO MASIKIN SIJUI MWAKA HUU NIFANYEJE TU.
at 7:58 am
Kiukweli loan board mna huruma it does not make sense mtu kasoma mpaka form six afu anashindwa kufuata masharti ya kujaza form? ilitakiwa wasipewe kabisa mkopo utasahauje kuweka sahihi yako na picha ya mzamini? why hawakusahau kupeleka form kutuma huu ni uzembe mkubwa sana hawa wasomi ni feki
at 9:42 am
JAMANI WATU WA BODI,MSITUTUPE WATU TULIOSOMA DIPLOMA,TUMESOMA KWA SHIDA SANA KAZI HAKUNA NYINYI MNALIJUA HILI,CHUO KIKUU ADA KUBWA SANA UKIJUMLISHA NA MICHANGO MINGINE,SIMNAONA MADAKTARI UNAWASOMESHA WENYEWE WANAWASUMBUA,WATU WA ARTS MSITUTUPE SISI TWENDE WAPI WATOTO WA KULIMAAAAAAAAA,HATA 20% TUTASHUKURU CHONDECHONDE JAMANI
at 4:18 pm
Bodi mnafanya kazi nzuri sasa.Saidieni vijana kuelewa kwa ufasaha vigezo vinavyotumika kuwapa mkopo mwaka huu.
at 2:20 pm
Mwaka huu itafahamika tu nani ni nani!
at 8:54 am
kwa kweli bod ya mikopo ituangalie yani kama mimi sijui nianzie wap niishie wap nasijui ntapata wapi hizo pesa za chuo tuangalieni na sisi watoto wa masikini jaman tusaidieni tupate japo hiyo digirii moja
at 9:33 am
2FIKIRIEN NA WATOTO WA WAKULIMA AMBAO HA2PENDI UALUM