Katibu wa UVCCM mkoa wa Singida Omary Mtua akitoa taarifa yake ya uchaguzi wa jumuiya ya vijana kwa mwandishi wa habari wa Mo Blog (hayupo kwenye picha). (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Jumla ya wanachama 38 wa jumuiya ya Umoja wa vijana CCM (UVCCM) mkoani Singida, wanagombea nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi wa jumuiya hiyo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Katibu wa UVCCM mkoani Singida Omary Mtua, amewataja Dinya Shabani Hamisi, Hamisi Haji Nkuwei, Heri Shabani Kundya, Labia Martin Zephania, Prince Antonio na Rehema Omari sombi, wanagombea nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM mkoa.
Amesema kwa upande wa nafasi ya mwenyekiti Singida mjini, nafasi hiyo imeombwa na Fikirini Hassan Salimu, Yasin Mdima, Ibrahimu Alli na Shaban Mhimbani.
Aidha Mtua amewataja Elia Sidadi, Shabani Mangola, Madiu Ndwete na Yohana Mnyangili kuwa wameomba nafasi ya uenyekiti wilaya ya Singida vijijini.
Katibu huyo amesema kwa upande wa wilaya mpya ya Ikungi, nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM imeombwa na Rebein Elisha Ibrahim (Anatetea nafasi yake), John Mughenyi, Joramu Ntandu, YOna Mwangu, Norman Mkola na Rajabu Njoha.
Amesema nafasi ya mwenyekiti UVCCM wilaya ya Manyoni, imeombwa na Omari Miraji, Faraji Idd, Emmanuel Chitambi, ANjelo Madundoo na Jane Likuda.
Aidha, amewataja Belinda Matalu, Juliana Zingula, Mary Mkoma Muungano Senyagwa na Athumani Rajabu, wameomba nafasi ya Mwenyekiti wa wilaya ya Iramba.
“Nafasi ya mwenyekiti UVCCM wilaya mpya ya Mkalama, imeombwa na Hamidu Omari, Jofiliki Mkwega, Joseph Saeda, Kiula Solomon na Sebastian Gunda”,amesema Mtua.
Wakati huo huo, Mtua amewataja Dinya Hamisi, Hansi Nkuwi, Preince Antonio na Saba saba Manase, wameomba nafasi ya mjumbe wa NEC kupitia tiketi ya mkoa wa SIngida kutoka UVCCM.
Amesema nafasi ya mjumbe wa baraza kuu taifa mkoa wa Singida, imeombwa na Heri Kundya, Dinya Hamisi, Joel Missanga, Jamila Kitila, Mazaba Warioba, Prince Antonio na Sabasaba Manase.








