WAISLAMU MKOANI SINGIDA WAHIMIZWA KUSHIRIKI SENSA YA TAIFA.

Katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida Salim Ngaa, akitoa salamu zake ya sherehe ya Eid Elfitiri  wakati wa sala ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa namfua mjini Singida.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Masambya akitoa nasaha zake wakati wa sala ya Idd Elfitiri iliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Imam wa msikiti wa Utemini mjini Singida, Jumanne Maulidi akisoma dua wakati wa sala ya Eid  Elfitiri iliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Baadhi ya waumini wa kiislamu waliohudhuria sala ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Sala hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.(Picha zote na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu

Katibu wa BAKWATA mkoa wa Singida,Salim Ngaa amewahimiza waislamu mkoani Singida kushiriki sensa ya taifa inayotarajiwa kufanyika nchini kote agosti 26 mwaka huu,kama njia moja wapo ya kuishukuru serikali kwa mema mengi inayoendelea kuwafanyia waislamu.

Ngaa ametoa wito huo (19/8/2012) wakati akizungumza kwenye sala ya Eid Eliftiri iliyofanyika kwenye uwanja wa michezo wa namfua mjini hapa.

Alisema lengo la serikali kuhesabu watu wake ni kutaka kujua idadi yao ili iwe rahisi kupanga mipango ya uhakika ya kuwaletea maendeleo pamoja na kutoa huduma zitakazokidhi mahitaji ya sehemu husika.

“Ndugu zangu waislamu tusidanganyike kwa lolote lile kuhusu zoezi hili la sensa ya mwaka huu.Tujitokeza wote kabisa na tutoe ushirikiano wa kutosha ili lengo la serikali liweze kufikiwa”,alisema Ngaa.

 
 
 

About the author

More posts by | Visit the site of Admin

 

 

 

Add a comment

required

required

optional