BINGWA WA MBIO ZA BAISKELI DUNIANI ARMSTRONG HATIANI KWA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU MICHEZONI.

Shirika la Kupambana na Matumizi ya Madawa Michezo nchini Marekani limechapisha ripoti inayoonesha sababu za kumpiga marufuku mshindi wa mbio za baiskeli  za Tour de France Lance Armstrong(pichani)  kutoshiriki mashindano hayo maishani.

Shirikahilo limesema kuna ushahidi wa kutosha unaothibitisha kwamba bingwa mara saba wa mbio za baiskeli duniani Lance Armstrong alihusika kwenye udanganyifu mkubwa kabisa wa kutumia madawa katika historia ya michezo.

 Ugunduzi wa shirika hilo umewasilishwa pia kwenye Chama cha Waendesha Baiskeli Duniani na Shirika la Kimataifa la Kupambana na Madawa ya Kuongeza Nguvu Michezoni.

Katika hatua nyingine George Hincapie mshirika wa timu ya Armstrong, ambaye alikuwa naye katika kila ushindi wake kwenye Tour de France tangu mwaka 1999 hadi 2005 amekiri kudanganya.  

 

 
 
 

About the author

More posts by

 

 

 

Add a comment

required

required

optional