Mwanamuziki wa kike Rehema Chalamila maarufu kama Ray C kwasasa anaishi maisha magumu baada ya kuathiriwa na kinachosemekana kuwa ni matumizi ya madawa ya kulevya kwa muda mrefu.
Mwanadada huyo maarufu kama kiuno bila mfupa hivi karibuni alihamishia makazi yake mjini Nairobi , Kenya, na aliporejea nchini hali yake ilikuwa mbaya.
Akizungumza na Mo blog kwa njia ya simu, mama mzazi wa Ray C, Bi Margret Mtweve amesikitishwa na kitendo cha vyombo vya habari kuandika tu hali ya Ray C bila kuhamasisha msaada..
“kwa kweli mwanagu ninae nyumbani kwasasa nalala nae kabisa, na nimeokoka namuombea sana kwa Mungu, na ninaamini Mungu ni mwema atamsaidia” alisema Bi Margret nakuongezea.
“Mwanangu aliwasaidia watu wengi lakini sasa hivi anamatatizo sioni mtu hata mmoja wakuja kunipa msaada, zaidi ni simu za waandishi kutaka habari za kumchafua”
Mama Ray C yuko tayari kupokea msaada wowote kutoka kwa wanajamii na namba yake ya simu ni 0655 999 700 waweza mtumia hata kwa Tigo Pesa.









at 11:20 am
a lesson in life to all of us.. Too much spot light can ruin you. Anyway its okay cause we all make mistakes in life
at 12:40 pm
inshallah mungu atamfanyia wepesi,namkumbuka enzi zile yuko clouds na me nafanya kazi zefona salamander.tutamuombea zaidi na kama si kiuwezo tkonae kimawazo,na kama si kimawazo bs ki uwezo
at 2:47 pm
Dah namuombea kwa mungu inshallah atapoa